An-Nisaa 4:54
النساءأَمْ يَحْسُدُونَ ٱلنَّاسَ عَلَىٰ مَآ ءَاتَىٰهُمُ ٱللَّهُ مِن فَضْلِهِۦ ۖ فَقَدْ ءَاتَيْنَآ ءَالَ إِبْرَٰهِيمَ ٱلْكِتَـٰبَ وَٱلْحِكْمَةَ وَءَاتَيْنَـٰهُم مُّلْكًا عَظِيمًا
Au wanawahusudu watu kwa yale aliyowapa Mwenyezi Mungu katika fadhila zake? Basi hakika tuliwapa ukoo wa Ibrahim Kitabu na hekima, na tukawapa ufalme mkubwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Au wanawahusudu watu kwa yale aliyo wapa Mwenyezi Mungu kwa fadhila yake? Basi tuliwapa ukoo wa Ibrahim Kitabu na hikima na tukawapa utawala mkubwa. [54]
[54] Na vipi watu hawa wanavyo waonea maya Waarabu? Na wakaona ni jambo kuu kuwa Mwenyezi Mungu alivyo wapa fadhila yake kwa kuwatolea Nabii kutokana nao, na ilhali Mwenyezi Mungu alimpa Ibrahim na ukoo wake - naye ni baba yenu (Mayahudi na Wakristo), na baba yao (Waislamu pia) - Kitabu kilicho teremshwa kwa ufunuo, na Unabii na Utawala ulio mkubwa!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Au je, kwani wao wanamhusudu Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie kwa neema za unabii na utume alizopewa na Allah Mtukufu na kuwahusudu Masahaba wake kwa neema ya kuongozwa kwenye Imani, kuukubali utume, kumfuata Mtume na kupewa uwezo katika ardhi, wakawa wanatamani neema hizi ziwaondokee? Hakika sisi tuliwapa watu wa kizazi cha Ibrãhîm, amani imshukie, Vitabu Alivyoviteremsha Allah Mtukufu kwao, wahyi mwingine usiokuwa kitabu chenye kusomwa na tukawapa, pamoja na hayo, utawala wenye kuenea.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net