Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 53

An-Nisaa 4:53

النساء

أَمْ لَهُمْ نَصِيبٌ مِّنَ ٱلْمُلْكِ فَإِذًا لَّا يُؤْتُونَ ٱلنَّاسَ نَقِيرًا

Maana

Au wanalo fungu katika mamlaka? Basi hapo wasingewapa watu hata jicho la kokwa ya tende.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Au wanayo sehemu ya utawala? Basi hapo wasingewapa watu hata tundu ya kokwa ya tende. [53]

[53] Hao wamekoseshwa neema ya kuifuata haki, kama walivyo koseshwa na utawala. Na lau wakipewa utawala hawanufaishi watu hata chembe.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Je, kwani wao wana fungu la ufalme? Na lau wangepewa, hawangalimpa yoyote kitu chochote katika hilo, hata kama ni kadiri ya kitone kilichoko kwenye koko ya tende.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net