Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 52

An-Nisaa 4:52

النساء

أُو۟لَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ لَعَنَهُمُ ٱللَّهُ ۖ وَمَن يَلْعَنِ ٱللَّهُ فَلَن تَجِدَ لَهُۥ نَصِيرًا

Maana

Hao ndio Mwenyezi Mungu amewalaani. Na ambaye Mwenyezi Mungu amemlaani, basi hutapata wa kumnusuru.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hao ndio Mwenyezi Mungu amewalaani. Na ambaye Mwenyezi Mungu amemlaani basi hutamwona kuwa na mwenye kumnusuru. [52]

[52] Hao ndio alio watupa Mwenyezi Mungu na akawafukuzilia mbali kutoka kwenye rehema yake. Na mwenye kutupwa na Mwenyezi Mungu na akatolewa kwenye rehema yake basi kabisa huyo hana wa kumnusuru na kumlinda na ghadhabu ya Mola wake Mlezi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hao ndio ambao umezidi uharibifu wao na umeenea upotevu wao. Allah Mtukufu,Aliyetukuka, Amewatoa kwenye rehema Yake. Na yoyote ambaye Allah Mtukufu Anamfukuza kwenye rehema Yake, hutampatia wa kumnusuru na kumuepushia adhabu mbaya.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net