Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 51

An-Nisaa 4:51

النساء

أَلَمْ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ نَصِيبًا مِّنَ ٱلْكِتَـٰبِ يُؤْمِنُونَ بِٱلْجِبْتِ وَٱلطَّـٰغُوتِ وَيَقُولُونَ لِلَّذِينَ كَفَرُوا۟ هَـٰٓؤُلَآءِ أَهْدَىٰ مِنَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ سَبِيلًا

Maana

Je, hukuwaona wale waliopewa fungu katika Kitabu? Wanaamini masanamu na Taghut! Na wanasema kuhusu wale waliokufuru kwamba hawa ndio walioongoka zaidi katika njia kuliko wale walioamini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Huwaoni wale walio pewa sehemu ya Kitabu? Wanaamini masanamu na Shet'ani! Na wanawasema walio kufuru, kuwa hao wameongoka zaidi katika njia kuliko Walio amini. [51]

[51] Hebu huwastaajabii hawa walio pewa sehemu ya ujuzi wa Kitabu wanavyo ridhia ibada ya masanamu na Shetani, na wanavyo sema kuwa hao waabuduo masanamu ni afadhali wameongoka kwenye Njia kuliko Waislamu wenye kuamini?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kwani hukujua, ewe Mtume, mambo ya wale Mayahudi waliopewa sehemu ya elimu, wanakiamini kila kiabudiwacho badala ya Allah Mtukufu, miongoni mwa masanamu na mashetani wa kibinadamu na wa kijini, imani inayowapelekea wao kuhukumiana kwa sheria isiyokuwa ya Allah Mtukufu, na wanasema kuwaambia wale waliomkufuru Allah Mtukufu, Aliyetukuka, na Mtume Wake Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukiye, «Hawa makafiri wako kwenye njia iliyo sawa zaidi na yenye uadilifu zaidi kuliko wale walioamini»?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net