Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 50

An-Nisaa 4:50

النساء

ٱنظُرْ كَيْفَ يَفْتَرُونَ عَلَى ٱللَّهِ ٱلْكَذِبَ ۖ وَكَفَىٰ بِهِۦٓ إِثْمًا مُّبِينًا

Maana

Tazama namna wanavyomzulia uongo Mwenyezi Mungu, na haya yanatosha kuwa dhambi iliyo wazi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Tazama vipi wanavyo mzulia uwongo Mwenyezi Mungu, na haya yatosha kuwa dhambi iliyo dhaahiri. [50]

[50] Vipi watu hawa wanavyo mzulia Mwenyezi Mungu uwongo kwa haya na mengineyo mfano wa haya! Yatosha uwovu ulio wazi kwa huu uwongo wao kuyakashifu maovu yao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Watazame, ewe Mtume, kwa kuyaonea ajabu mambo yao, vipi wanamzulia Allah Mtukufu urongo, na hali Yeye Ndiye Anayetakaswa na kila lisilolingana na utukufu wake Uzushi huu unatosha kuwa ni dhambi kubwa lenye kuonyesha wazi itikadi yao mbovu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net