Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 49

An-Nisaa 4:49

النساء

أَلَمْ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ يُزَكُّونَ أَنفُسَهُم ۚ بَلِ ٱللَّهُ يُزَكِّى مَن يَشَآءُ وَلَا يُظْلَمُونَ فَتِيلًا

Maana

Je, hukuwaona wale wanaojitakasa nafsi zao? Bali Mwenyezi Mungu humtakasa amtakaye. Na hawatadhulumiwa hata kiasi cha kijiuzi kilicho ndani ya uwazi wa kokwa ya tende.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Jee huwaoni wale wanao dai kuwa ati wametakasika? Bali Mwenyezi Mungu humtakasa amtakaye. Na hawatadhulumiwa hata kadiri ya kijiuzi kilichomo ndani ya uwazi wa kokwa ya tende. [49]

[49] Hustaajabii hali ya hao makafiri wanao zua kwa vitendo vyao? Vitendo vyao viovu wao wanaviona kuwa ni vizuri. Wanajisifu kuwa kwa vitendo hivyo wao wametakasika. Na ni Mwenyezi Mungu tu peke yake ndiye anaye jua jema na baya. Yeye ndiye wa kumtakasa amtakaye, na wala hamdhulumu mtu yeyote kadiri yake hata chembe.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kwani hukujua, ewe Mtume, hali ya wale wanaojisifu wenyewe na kuyasifu matendo yao kuwa yametakasika na kuwa yako mbali na uovu? Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Peke Yake Ndiye Ambaye Anamsifu Amtakaye miongoni mwa waja Wake, kwa kuwa Yeye Ndiye ajuae ukweli wa matendo yao. Na wala hawatapunguziwa chochote katika matendo yao, hata kama ni kadiri ya uzi ulio kwenye mwanya wa koko ya tende.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net