Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 48

An-Nisaa 4:48

النساء

إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِۦ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَآءُ ۚ وَمَن يُشْرِكْ بِٱللَّهِ فَقَدِ ٱفْتَرَىٰٓ إِثْمًا عَظِيمًا

Maana

Hakika, Mwenyezi Mungu hafuti dhambi ya kushirikishwa, na hufuta dhambi ya yale yaliyo duni ya hilo kwa amtakaye. Na mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu, basi hakika amezua dhambi kubwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika Mwenyezi Mungu hasamehe kushirikishwa, na husamehe yaliyo duni ya hilo kwa amtakaye. Na anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu basi hakika amezua dhambi kubwa. [48]

[48] Hakika Mwenyezi Mungu hafuti dhambi za ushirikina, kumfanya Yeye ana mshirika yeyote. Na husamehe dhambi zilio chini ya huo ushirikina kwa amtakaye miongoni mwa waja wake. Na mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu basi amemzulia Mwenyezi Mungu na ametenda dhambi kubwa mno isiyo stahiki kusamehewa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Hamsamehe aliyemshirikisha Yeye na yoyote miongoni mwa viumbe Wake au akamkufuru kwa aina yoyote ya ukafiri mkubwa. Lakini Anayasamehe na kuyafuta madhambi yaliyo chini ya ushirikina kwa Anayemtaka miongoni mwa waja Wake. Na yoyote anayemshirikisha Allah Mtukufu na mwingine, hakika amefanya dhambi kubwa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net