An-Nisaa 4:47
النساءيَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ ٱلْكِتَـٰبَ ءَامِنُوا۟ بِمَا نَزَّلْنَا مُصَدِّقًا لِّمَا مَعَكُم مِّن قَبْلِ أَن نَّطْمِسَ وُجُوهًا فَنَرُدَّهَا عَلَىٰٓ أَدْبَارِهَآ أَوْ نَلْعَنَهُمْ كَمَا لَعَنَّآ أَصْحَـٰبَ ٱلسَّبْتِ ۚ وَكَانَ أَمْرُ ٱللَّهِ مَفْعُولًا
Enyi mliopewa Kitabu! Aminini tuliyoyateremsha yenye kusadikisha yale mliyo nayo, kabla hatujazifutilia mbali nyuso na kuzipeleka nyuma yake, au tuwalaani kama tulivyowalaani watu wa Sabato (Jumamosi). Na amri ya Mwenyezi Mungu ni lazima ifanyike.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Enyi mlio pewa Kitabu! Aminini tuliyo yateremsha yenye kusadikisha yale mliyo nayo, kabla hatujazigeuza nyuso tukazipeleka kisogoni, au tukawalaani kama tulivyo walaani watu wa Sabato (Jumaamosi). Na amri ya Mwenyezi Mungu ni lazima ifanyike. [47]
[47] Enyi mlio pewa Kitabu alicho teremsha Mwenyezi Mungu! Iaminini Qur'ani tuliyo mteremshia Muhammad, inayo sadikisha mliyo nayo, kabla hatujawateremshia adhabu ya kufutwa nyuso zenu zikawa kama visogo, hazina pua, wala macho, wala nyusi. Au tukakutoeni katika rehema yetu kama tulivyo watoa wale walio ikhalifu amri yetu wakatenda waliyo katazwa ya kuvua samaki siku ya mapumziko,(Sabt au Sabato) siku ya Jumaamosi. Na hukumu ya Mwenyezi Mungu ni yenye kutimizwa tu, wala hapana cha kuipinga.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Enyi watu wa Kitabu, Aminini na mufuate kivitendo yale tuliyoyateremsha kwenye Qur’ani, yenye kusadikisha Vitabu vilivyoko kwenu, kabla hatujawaadhibu kwa matendo yenu mabaya tukazifuta nyuso na kuzigeuza upande wa migongo au tukawapa laana waharibifu hawa kwa kuwageuza kuwa manyani na nguruwe, kama tulivyowapa laana watu wa Jumamosi ambao walikatazwa kuvua siku hii wakapinga, Allah Mtukufu Akawakasirikia na Akawafukuza kutoka kwenye rehema Yake. Na amri ya Allah Mtukufu ni yenye kupita kwa hali yoyote.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net