An-Nisaa
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ بِـَٔايَـٰتِنَا سَوْفَ نُصْلِيهِمْ نَارًا كُلَّمَا نَضِجَتْ جُلُودُهُم بَدَّلْنَـٰهُمْ جُلُودًا غَيْرَهَا لِيَذُوقُوا۟ ٱلْعَذَابَ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَزِيزًا حَكِيمًا 56
{56} Na ndiyo maana akasema, “Hakika wale waliozikufuru Ishara zetu, tutawaingiza motoni,” yani wenye kuni kubwa, na joto kali. “Kila zitakapoiva ngozi zao,” yani zitakapochomeka, “tutawabadilishia ngozi nyingine ili waionje hiyo adhabu.” Yani ili adhabu iwafike kila penye kufika. Na kama vile ukafiri wao na ukaidi wao ulivyorudia, na yakawa ndiyo sifa yao na tabia yao, atawarudia adhabu kama malipo mwafaka. Na kwa sababu hiyo akasema, “Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.” Yani ana Nguvu nyingi, na hekima katika uumbaji wake, na amri, na thawabu zake, na adhabu.