Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 65

An-Nisaa 4:65

النساء

فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا۟ فِىٓ أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Maana

Hapana! Ninaapa kwa Mola wako Mlezi! Hawataamini mpaka wakufanye wewe ndiye mwenye kuhukumu katika yale wanayohitilafiana, kisha wasipate uzito wowote katika nyoyo zao juu ya hukumu utakayotoa, na wajisalimishe kujusalimisha kukamilifu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

La! Naapa kwa Mola wako Mlezi! Hawataamini mpaka wakufanye wewe ndiye muamuzi katika yale wanayo khitalifiana, kisha wasione uzito katika nyoyo zao juu ya hukumu utayo toa, na wanyenykee kabisa. [65]

[65] Naapa kwa jina la Mola wako Mlezi! Hawahisabiwi kuwa ni Waumini wa Haki na wenye kuinyenyekea, mpaka watakapo kufanya wewe hakimu muamuzi wa mizozo inayo tokea baina yao. Kisha nafsi zao zisione dhiki kwa utavyo hukumu, na wakunyenyekee kama wanavyo nyenyekea Waumini wa kweli.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu Anaapa kwa nafsi Yake tukufu, kwamba hawa hawataamini kikweli mpaka wakufanye wewe ni hakimu kwenye ugomvi unaotokea baina yao katika uhai wako na watake uamuzi wa Sunnah yako baada ya kufa kwako, kisha wasiingiwe na dhiki katika nafsi zao kwa matokeo ya hukumu yako, na wakufuate, pamoja na hivyo, kukufuata kikamilifu. Kutoa uamuzi kulingana na aliyokuja nayo Mtume wa Allah Mtukufu, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukiye, kutoka kwenye Qur’ani na Sunnah katika kila jambo katika mambo ya kimaisha, pamoja na kuridhika na kusalimu amri, ni miongoni mwa uthabiti Imani

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net