An-Nisaa 4:66
النساءوَلَوْ أَنَّا كَتَبْنَا عَلَيْهِمْ أَنِ ٱقْتُلُوٓا۟ أَنفُسَكُمْ أَوِ ٱخْرُجُوا۟ مِن دِيَـٰرِكُم مَّا فَعَلُوهُ إِلَّا قَلِيلٌ مِّنْهُمْ ۖ وَلَوْ أَنَّهُمْ فَعَلُوا۟ مَا يُوعَظُونَ بِهِۦ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُمْ وَأَشَدَّ تَثْبِيتًا
Na lau kuwa tuliwaandikia kuwa: 'Jiueni, au tokeni majumbani mwenu', wasingeliyafanya hayo isipokuwa wachache tu miongoni mwao. Na lau kama wangeliyafanya yale wanayowaidhiwa kwayo, ingelikuwa bora kwao na uthibitisho wa nguvu zaidi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na lau kuwa tumewaamrisha: Jiueni, au tokeni majumbani kwenu, wasingeli fanya hayo ila wachache tu miongoni mwao. Na lau kama wangeli fanya walio waidhiwa ingeli kuwa bora kwao na uthibitisho wa nguvu zaidi. [66]
[66] Na lau kuwa Sisi tumewalazimisha mashaka ya mwisho, kwa kuwaamrisha wapigane Jihadi moja kwa moja, na wajitolee nafsi zao kutilifu, au watoke nje waache majumba yao kwenda pigana Jihadi daima, wasinge kubali kut'ii ila wachache tu. Lakini Mwenyezi Mungu, Aliye takasika na kutukuka, hakalifishi ila linalo wezekana. Na lau kuwa wange fanya hayo na wakafuata haki yake ingeli kuwa ni kheri yao ya duniani na Akhera. Na hivyo ndiyo inavyo pelekea kuthibiti Imani, na kuingia imara, na kuleta utulivu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na lau tungewalazimisha wanafiki hawa, wenye kuhukumiana kwa ṭãghût (sheria zisizokuwa za Allah Mtukufu), wauane wao kwa wao au watoke kwenye majumba yao, hawangalifuata amri hiyo isipokuwa wachache katika wao. Na lau kwamba wao wangekubali nasaha walizonasihiwa, hilo lingalikuwa ni lenye kuwanufaisha na ni lenye kutia nguvu zaidi Imani yao,
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net