Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 44

An-Nisaa 4:44

النساء

أَلَمْ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ نَصِيبًا مِّنَ ٱلْكِتَـٰبِ يَشْتَرُونَ ٱلضَّلَـٰلَةَ وَيُرِيدُونَ أَن تَضِلُّوا۟ ٱلسَّبِيلَ

Maana

Je, hukuwaona wale waliopewa fungu katika Kitabu wanaununua upotovu na wanataka kwamba mpotee Njia?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Huwaoni wale waliopewa sehemu ya Kitabu wananunua upotovu na wanakutakeni nanyi mupotee Njia? [44]

[44] Hebu huyastaajabii mambo ya hawa walio pewa sehemu ya Vitabu vilivyo tangulia wanavyo acha uwongofu na wakatafuta upotovu katika mambo yaliyo wakhusu nafsi zao! Na wao tena wanakutakeni nyinyi mjitenge na Haki ambayo ndiyo Njia ya Mwenyezi Mungu Iliyo Nyooka!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kwani hukujua, ewe Mtume, mambo ya Mayahudi waliopewa fungu la elimu kwa Taurati iliyowajia, wanatoa uongofu na kuchukua upotevu badala yake, wanaacha hoja na dalili walizonazo zenye kuonesha ukweli wa ujumbe wa Mtume Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukiye, na wanawatakia nyinyi, enyi Waumini, muende kombo na njia iliyolingana ili muwe wapotevu kama wao?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net