Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 43

An-Nisaa 4:43

النساء

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَا تَقْرَبُوا۟ ٱلصَّلَوٰةَ وَأَنتُمْ سُكَـٰرَىٰ حَتَّىٰ تَعْلَمُوا۟ مَا تَقُولُونَ وَلَا جُنُبًا إِلَّا عَابِرِى سَبِيلٍ حَتَّىٰ تَغْتَسِلُوا۟ ۚ وَإِن كُنتُم مَّرْضَىٰٓ أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ أَوْ جَآءَ أَحَدٌ مِّنكُم مِّنَ ٱلْغَآئِطِ أَوْ لَـٰمَسْتُمُ ٱلنِّسَآءَ فَلَمْ تَجِدُوا۟ مَآءً فَتَيَمَّمُوا۟ صَعِيدًا طَيِّبًا فَٱمْسَحُوا۟ بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُمْ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَفُوًّا غَفُورًا

Maana

Enyi mlioamini! Msiikaribie Swala hali ya kuwa mmelewa, mpaka myajue mnayoyasema. Wala mkiwa na janaba (msikaribie swala wala msikiti), isipokuwa wanaopita njia (msikitini), mpaka muoge. Na mkiwa wagonjwa, au katika safari, au mmoja wenu akitoka chooni, au mkiwagusa (yaani kuwajamii) wanawake, na msipate maji, basi ukusudieni mchanga safi. Basi upangusieni kwenye nyuso zenu na mikono yenu. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Msamehevu, Mwenye kufuta dhambi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi mlio amini! Msikaribie Sala, hali mmelewa, mpaka myajue mnayo yasema, wala hali mna janaba - isipo kuwa mmo safarini - mpaka mkoge. Na mkiwa wagonjwa, au mmo safarini, au mmoja wenu ametoka chooni, au mmewagusa wanawake - na msipate maji, basi ukusudieni mchanga safi, mpake nyuso zenu na mikono yenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Msamehevu na Mwenye kughufiria. [43]

[43] Enyi mlioamini! Msende kusali misikitini nanyi mmo katika hali ya ulevi mpaka muwe mnafahamu myasemayo. Wala msiingie misikitini nanyi mna janaba, ila ikiwa ni kupita njia tu bila ya kusita, mpaka mtahirike kwa kukoga. Na mkiwa ni wagonjwa hamuwezi kutumia maji kwa kuogopa maradhi yasikuzidini au kuchelewa kupona, au mkiwa mmo safarini na ipo shida ya kupata maji, basi tumieni mchanga ulio safi. Kadhaalika mmoja wenu akitoka chooni, au mkawaingilia wanawake na mkawa hamkupata maji ya kujitahirishia kwa kukosekana kwake, basi vile vile chukueni mchanga safi upigeni kwa mikono yenu, na mpangusie nyuso zenu na mikono yenu. Hakika ni shani ya Mwenyezi Mungu kuwa ni Mwenye kusamehe sana na Mwenye kufuta dhambi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi ambao mlimuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkafuata Sheria Yake kivitendo, msiikaribie Swala wala msisimame kwenda kusali mkiwa katika hali ya ulevi mpaka muyaelewe na muyajue mnayoyasema. -Hii ilikuwa kabla ya kuthibitishwa uharamu wa pombe katika hali zote-.Na wala msikaribie Swala mkiwa na hadathi kubwa, nayo ni janaba. Na pia, mkiwa na janaba, msizikaribie sehemu za Swala, nazo ni misikiti, isipokuwa kwa mpita njia, katika nyinyi, kutoka kwenye mlango hadi mlango mwingine, mpaka mjitwahirishe kwa kuoga. Na mkiwa katika hali ya ugonjwa, mkawa hamuwezi kutumia maji, au hali ya safari, au mmoja wenu akaja kutoka kwenye haja kubwa au ndogo au mkawaingilia wanawake na msipate maji ya kujisafisha, ujieni mchanga uliyo tohara mjipanguse nao nyuso zenu na mikono yenu. Allah Mtukufu ni Mwingi wa msamaha, Anayasamehe makosa yenu na Anawasitiria.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net