Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 42

An-Nisaa 4:42

النساء

يَوْمَئِذٍ يَوَدُّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ وَعَصَوُا۟ ٱلرَّسُولَ لَوْ تُسَوَّىٰ بِهِمُ ٱلْأَرْضُ وَلَا يَكْتُمُونَ ٱللَّهَ حَدِيثًا

Maana

Siku hiyo watapenda wale waliokufuru na wakamuasi Mtume lau kuwa ardhi isawazishwe kwa wao. Wala hawataweza kumficha Mwenyezi Mungu neno lolote.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Siku hiyo walio kufuru na wakamuasi Mtume watatamani Ardhi isawazishwe juu yao. Wala hawataweza kumficha Mwenyezi Mungu neno lolote. [42]

[42] Yatapo tokea haya watatamani hao wapinzani wanao pinga lau kuwa wangeli potea chini ya Ardhi kama wanavyo potea maiti makaburini! Na wao hawawezi kumficha Mwenyezi Mungu kitu chochote katika mambo yao, na hali zao na vitendo vyao vitadhihiri.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Siku litakapokuwa hilo, watatamani, wale waliomkanusha Allah Mtukufu, Aliyetukuka, na wakampinga Mtume wasimtii, lau Allah Mtukufu Angaliwafanya sawasawa, wao na ardhi, wakawa mchanga ili wasifufuliwe. Na wao hawawezi kumficha Allah Mtukufu chochote kilichoko ndani ya nafsi zao, kwa kuwa Allah Mtukufu Atakuwa Amefunga midomo yao na kutolewa ushahidi juu yao na viungo vyao wenyewe kwa yale waliokuwa wakiyafanya.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net