Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 41

An-Nisaa 4:41

النساء

فَكَيْفَ إِذَا جِئْنَا مِن كُلِّ أُمَّةٍۭ بِشَهِيدٍ وَجِئْنَا بِكَ عَلَىٰ هَـٰٓؤُلَآءِ شَهِيدًا

Maana

Basi itakuwa vipi tutakapoleta shahidi kutoka kwa kila umma, na tukakuleta wewe kuwa shahidi dhidi ya hawa?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi itakuwaje pindi tukiwaletea kutoka kila umma shahidi, na tukakuleta wewe kuwa shahidi wa hawa? [41]

[41] Vipi basi itakuwa hali ya hao mabakhili wanao pingana na aliyo yaamrisha Mwenyezi Mungu, tutapo mleta Siku ya Kiyama kila Nabii awe ni shahidi juu ya kaumu yake, na tukakuleta wewe, ewe Nabii Muhammad, kuwa ni shahidi juu ya kaumu yako, na hali miongoni mwao wapo hao wanao zuia mali yao na wanao pinga?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Vipi itakuwa hali ya watu, Siku ya Kiyama, pindi Allah Mtukufu Atakapomleta Mtume wa kila ummah, ili atoe ushahidi juu yake kwa yale uliyoyafanya, na atakapo kuleta wewe, ewe Mtume, utoe ushahidi juu ya ummah wako kwamba wewe uliwafikishia ujumbe wa Mola wako?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net