Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 40

An-Nisaa 4:40

النساء

إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَظْلِمُ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ ۖ وَإِن تَكُ حَسَنَةً يُضَـٰعِفْهَا وَيُؤْتِ مِن لَّدُنْهُ أَجْرًا عَظِيمًا

Maana

Hakika Mwenyezi Mungu hadhulumu hata uzito wa chembe moja. Na ikiwa ni jambo zuri, atalizidisha na atapeana kutoka kwake malipo makubwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika Mwenyezi Mungu hadhulumu hata uzito wa chembe moja. Na ikiwa ni jambo jema basi Yeye hulizidisha na hutoa kutoka kwake malipo makubwa. [40]

[40] Hakika Mwenyezi Mungu hamdhulumu mtu hata kidogo. Basi hampunguzii ujira wake mtu, wala adhabu yake hamzidishii kabisa. Bali humzidishia mtenda mema thawabu zake mardufu hata zikiwa kidogo vipi. Na humpa kwa fadhila yake malipo makubwa yasiyo lingana na hayo mema yake ambayo yamekwisha zidishwa mardufu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu Hampunguzii yoyote malipo ya matendo yake hata kama ni kadiri ya chungu. Na uwapo huo uzito wa chungu ni jambo jema, basi Allah Mtukufu, Aliyetakasika na sifa pungufu, Atamuongezea na kumkuzia mwenye kulifanya, na Atamkirimu kwa nyongeza, kwa kumpa kutoka Kwake thawabu kubwa ambazo ni Pepo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net