Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 39

An-Nisaa 4:39

النساء

وَمَاذَا عَلَيْهِمْ لَوْ ءَامَنُوا۟ بِٱللَّهِ وَٱلْيَوْمِ ٱلْـَٔاخِرِ وَأَنفَقُوا۟ مِمَّا رَزَقَهُمُ ٱللَّهُ ۚ وَكَانَ ٱللَّهُ بِهِمْ عَلِيمًا

Maana

Na ingeliwadhuru nini wao lau wangelimwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na wakatoa katika yale aliyowaruzuku Mwenyezi Mungu? Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwajua vyema.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na ingeli wadhuru nini wao lau wangeli muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na wakatoa katika aliyo waruzuku Mwenyezi Mungu? Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwajua vyema. [39]

[39] Ama wamelaanika watu hawa! Kingewadhuru nini wao lau kuwa wamemuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Akhera, na wakatoa katika alicho wapa Mwenyezi Mungu kwa kufuatana na Imani hii, na usafi wa niya, na kutaraji thawabu kama ilivyo wajibikia? Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua kwa ujuzi kaamili mambo yote yaliyo wazi na yaliyo fichikana ndani.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kwani kuna madhara gani yatakayowafika wao lau wangemuamini Allah Mtukufu na Siku ya Mwisho, kiitikadi na kivitendo, na wakayatoa yale Aliyowapa Allah Mtukufu kwa kutaka thawabu na kuwa na ikhlasi. Allah Mtukufu ni Mjuzi wa kuwajua wao na kuyajua wayafanyayo na Atawahesabu kwayo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net