An-Nisaa 4:38
النساءوَٱلَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَٰلَهُمْ رِئَآءَ ٱلنَّاسِ وَلَا يُؤْمِنُونَ بِٱللَّهِ وَلَا بِٱلْيَوْمِ ٱلْـَٔاخِرِ ۗ وَمَن يَكُنِ ٱلشَّيْطَـٰنُ لَهُۥ قَرِينًا فَسَآءَ قَرِينًا
Na ambao hutoa mali zao ili kujionyesha kwa watu, wala hawamwamini Mwenyezi Mungu wala Siku ya Mwisho. Na yule ambaye Shetani amekuwa ndiye mwenza wake, basi ana mwenza mbaya mno.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na ambao hutoa mali yao kwa kuonyesha watu, wala hawamuamini Mwenyezi Mungu wala Siku ya Mwisho; na yule ambaye Shet'ani amekuwa ndiye rafiki yake, basi ana rafiki mbaya mno. [38]
[38] Na Mwenyezi Mungu hawapendi wanao toa mali kwa ajili ya kuonekana na watu, wapate kuwasifu na kuwatukuza, na ilhali wao si wenye kumuamini Mwenyezi Mungu wala Siku ya Malipo. Kwani hao wamemfuata Shetani naye amewapoteza. Na mwenye kuwa rafiki yake ni Shetani basi ana rafiki mbaya kweli.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na pia tumewaandalia adhabu hii wale ambao wanatoa mali yao kwa njia ya ria na kujitangaza na hawamuamini Allah Mtukufu, kiitikadi na kivitendo, wala Siku ya Kiyama. Matendo haya mabaya ni miongoni mwa yale yanayolinganiwa na Shetani. Na yoyote yule ambaye Shetani atakuwa ni mwenye kushikamana na yeye, basi mtu mbaya wa kushikamana naye na kufanya naye urafiki ni yeye.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net