Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 37

An-Nisaa 4:37

النساء

ٱلَّذِينَ يَبْخَلُونَ وَيَأْمُرُونَ ٱلنَّاسَ بِٱلْبُخْلِ وَيَكْتُمُونَ مَآ ءَاتَىٰهُمُ ٱللَّهُ مِن فَضْلِهِۦ ۗ وَأَعْتَدْنَا لِلْكَـٰفِرِينَ عَذَابًا مُّهِينًا

Maana

Ambao wanafanya ubahili na wanaamrisha watu ubahili, na wanaficha yale aliyowapa Mwenyezi Mungu katika fadhila zake. Na tuliwaandalia makafiri adhabu ya kudunisha.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ambao wanafanya ubakhili na wanaamrisha watu ubakhili, na wanaficha fadhila alizo wapa Mwenyezi Mungu. Na tumewaandalia makafiri adhabu ya fedheha, [37]

[37] Hao ndio wanao ongeza juu ya takaburi na tafakhuri yao ila ya kuwafanyia watu ubakhili kwa mali yao na juhudi yao. Tena ikawa wanawataka watu wafanye ubakhili kama wao. Kazi yao ni kukhofia neema na fadhila ya Mwenyezi Mungu isiwatoke. Kwa hivyo, basi, hawajifai wenyewe wala hawawafai watu. Wapinzani kama hao tumekwisha waandalia adhabu ya kutia machungu na ya kudhalilisha.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Nao ni wale wanaojizuia kutumia na kutoa kile Alichowaruzuku Allah Mtukufu, wakawaamuru wengineo kufanya ubahili, wakazikanusha neema za Allah Mtukufu juu yao na wakazificha fadhila Zake na vipewa Vyake. Na tumewaandalia wenye kukanusha adhabu yenye kudhalilisha.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net