An-Nisaa 4:36
النساءوَٱعْبُدُوا۟ ٱللَّهَ وَلَا تُشْرِكُوا۟ بِهِۦ شَيْـًٔا ۖ وَبِٱلْوَٰلِدَيْنِ إِحْسَـٰنًا وَبِذِى ٱلْقُرْبَىٰ وَٱلْيَتَـٰمَىٰ وَٱلْمَسَـٰكِينِ وَٱلْجَارِ ذِى ٱلْقُرْبَىٰ وَٱلْجَارِ ٱلْجُنُبِ وَٱلصَّاحِبِ بِٱلْجَنۢبِ وَٱبْنِ ٱلسَّبِيلِ وَمَا مَلَكَتْ أَيْمَـٰنُكُمْ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُحِبُّ مَن كَانَ مُخْتَالًا فَخُورًا
Na mwabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni wema wazazi wawili, na jamaa, na mayatima, na masikini, na jirani wa karibu, na jirani wa ubavuni, na mwenza wa ubavuni, na mwana njia, na wale iliowamiliki mikono yenu ya kulia. Hakika, Mwenyezi Mungu hampendi mwenye kiburi anayejifahiri.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Muabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni wema wazazi wawili na jamaa na mayatima na masikini na jirani wa karibu na jirani wa mbali, na rafiki wa ubavuni na mpita njia, na walio milikiwa na mikono yenu ya kulia. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wenye kiburi wanao jifakhiri, [36]
[36] Nanyi muabuduni Mwenyezi Mungu peke yake, wala msimfanyie washirika katika Ungu na kuabudiwa. Na watendeeni wema wazazi wenu bila ya taksiri yoyote, na pia jamaa zenu, na mayatima, na walio fakirika kwa sababu ya kuemewa au kupata masaibu katika mali yao, na jirani mliye karibiana naye kwa nasaba, na jirani mtu mbali, na mwenzio katika kazi au njia au majlisi, na msafiri mhitaji asiye kuwa na kituo katika nchi maalumu, na watumwa wenu wanaume na wanawake mlio wamiliki. Hakika Mwenyezi Mungu hampendi anaye jipa ubora juu ya watu wengine, na hawachukulii watu kwa huruma, na anakithirisha kujisifu mwenyewe kwa kujifakhiri.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na muabuduni Allah Mtukufu na mtiini Yeye Peke Yake, wala msimfanyie mshirika katika ustahiki wa kuwa Ndiye Mola na Ndiye Mwenye kuabudiwa, na wafanyieni wema wazazi wawili na mtekeleze haki zao na haki za jamaa wa karibu, na mayatima na wahitaji, na jirani wa karibu na wa mbali, na rafiki wa safari na wa mjini, na msafiri mwenye uhitaji, na waliomilikiwa na nyinyi, wanaume na wanawake. Hakika Allah Mtukufu Hawapendi, katika waja Wake, wenye kiburi na kujigamba kwa watu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net