An-Nisaa 4:35
النساءوَإِنْ خِفْتُمْ شِقَاقَ بَيْنِهِمَا فَٱبْعَثُوا۟ حَكَمًا مِّنْ أَهْلِهِۦ وَحَكَمًا مِّنْ أَهْلِهَآ إِن يُرِيدَآ إِصْلَـٰحًا يُوَفِّقِ ٱللَّهُ بَيْنَهُمَآ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلِيمًا خَبِيرًا
Na mkihofia kuwepo mfarakano baina ya wawili hao, basi mtumeni mpatanishi kutoka kwa jamaa za mume, na mpatanishi kutoka kwa jamaa za mke. Ikiwa wanataka kutengeneza mambo, Mwenyezi Mungu ataleta maafikiano kati yao. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye habari zote.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na mkichelea kutakuwapo mfarakano baina ya mke na mume basi pelekeni muamuzi kutokana na jamaa za mume, na muamuzi kutokana na jamaa za mke. Wakitaka mapatano Mwenyezi Mungu atawawezesha. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye khabari. [35]
[35] Pindi pakitokea kukhitalifiana baina ya mke na mume, na mkakhofia kutokea kufarikiana kutako leta t'alaka, chagueni waamuzi wawili. Mmoja kutokana na upande wa mume na mwengine upande wa mke. Wakitaka kusuluhiana Mwenyezi Mungu atawawafikisha wafikilie lilio kheri kwa wote wawili, nako ama kukaa kwa wema au kuachana kwa ihsani. Hakika Mwenyezi Mungu anachungua kila kitu cha waja wake, kilicho dhihiri na kilicho fichikana.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na mkijua, enyi wasimamizi wa mume na mke, kuwa kuna ugomvi baina yao unaopelekea kutengana, wapelekeeni mwamuzi muadilifu wa upande wa mume na mwamuzi muadilifu wa upande wa mke, ili watazame na kutoa uamuzi wenye maslahi ya wao wawili. Na kwa kuwa wale waamuzi wawili wana hamu ya kupatanisha na wanatumia njia nzuri, Allah Mtukufu Atawatilia taufiki baina ya mume na mke. Allah Mtukufu ni Mjuzi, hakuna chochote kinachofichamana Kwake kuhusu mambo ya waja Wake, ni Mtambuzi wa yaliyomo ndani ya nafsi zao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net