An-Nisaa 4:34
النساءٱلرِّجَالُ قَوَّٰمُونَ عَلَى ٱلنِّسَآءِ بِمَا فَضَّلَ ٱللَّهُ بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ وَبِمَآ أَنفَقُوا۟ مِنْ أَمْوَٰلِهِمْ ۚ فَٱلصَّـٰلِحَـٰتُ قَـٰنِتَـٰتٌ حَـٰفِظَـٰتٌ لِّلْغَيْبِ بِمَا حَفِظَ ٱللَّهُ ۚ وَٱلَّـٰتِى تَخَافُونَ نُشُوزَهُنَّ فَعِظُوهُنَّ وَٱهْجُرُوهُنَّ فِى ٱلْمَضَاجِعِ وَٱضْرِبُوهُنَّ ۖ فَإِنْ أَطَعْنَكُمْ فَلَا تَبْغُوا۟ عَلَيْهِنَّ سَبِيلًا ۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلِيًّا كَبِيرًا
Wanaume ni wasimamizi imara wa wanawake, kwa yale aliyowafadhilisha kwayo Mwenyezi Mungu baadhi yao juu ya baadhi, na kwa yale wanayoyatoa katika mali zao. Basi wanawake wema ni wale wenye kutii na wanaojilinda hata katika siri kwa kuwa Mwenyezi Mungu ameamrisha wajilinde. Na wale mnaochelea kutoka kwao katika utiifu, waaidhini, na wahameni katika malazi, na wapigeni. Basi wakiwatii, msitafute njia yoyote dhidi yao. Hakika, Mwenyezi Mungu ndiye aliye juu, Mkubwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wanaume ni wasimamizi wa wanawake, kwa kufadhiliwa na Mwenyezi Mungu baadhi yao juu ya baadhi, na kwa mali yao wanayo yatoa. Basi wanawake wema ni wale wenye kut'ii na wanao jilinda hata katika siri kwa kuwa Mwenyezi Mungu ameamrisha wajilinde. Na ambao mnachelea kutoka katika ut'iifu wanasihini, muwahame katika malazi na wapigeni. Wakikut'iini msiwatafutie njia ya kuwaudhi bure. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye aliye juu na Mkuu. [34]
[34] Wanaume wana haki ya kuwaangalia na kuwachunga wanawake, na kuwasimamia katika mambo yao kwa vile Mwenyezi Mungu amewapa wao wanaume sifa za kuweza kuisimamia haki hii, na kwa kuwa wao ndio wanao hangaika na kufanya juhudi ya kutafuta mali ya kuutumilia ukoo mzima. Basi wanawake wema wanakuwa ni wat'iifu kwa Mwenyezi Mungu na waume zao. Ni wenye kuhifadhi vyote ambavyo waume zao hawavioni kwa sababu Mwenyezi Mungu ameamrisha vihifadhiwe, na kwa kuwapa wao tawfiki. Na wanawake wanao onyesha kuanza uasi wanasihini kwa maneno yenye kuathiri. Kama hawakusikia tenganeni nao kitandani. Hawakusikia, watieni adabu kwa pigo dogo, si la kuwajuruhi wala kuwadhalilisha. Wakirejea kwenye ut'iifu wenu kwa njia mojapo katika hizi tatu basi msiwatafutie kisababu cha kuwatesa zaidi kuliko haya. Hakika Mwenyezi Mungu yuko juu yenu, naye atakupatilizeni pindi mkiwaudhi wake zenu au mkawafanyia jeuri.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wanaume ni wasimamizi wa kuwaelekeza wanawake na kuwatunza, kwa kile ambacho Allah Mtukufu Amewatunuku nacho cha sifa za usimamizi na kutukuzwa, na mahari na matumizi waliyowapa hao wanawake. Basi wale walio wema katika wao, hao wanawake, kwa kuhifadhiwa na Allah Mtukufu na kuafikiwa, wanasimama imara kufuata sheria ya Allah Mtukufu, wanamtii Allah Mtukufu, Aliyetukuka, na wanatunza kila lisilojulikana na waume zao katika mambo waliyoaminiwa nayo. Na wale katika wao mnaochelea kuwafanyia nyinyi ujeuri kwa kuacha kuwatii, wapeni nasaha kwa maneno mazuri; iwapo maneno mazuri hayakuzaa matunda kwao, wahameni vitandani wala msiwakaribie. Iwapo kuwahama hakukuwafanya waathirike na kubadili mwenendo wao, basi wapigeni kipigo kisicho na madhara. Na wakiwa watawatii, jihadharini kuwafanyia maonevu. Kwani Mwenye zi Mungu Aliye juu, Aliye Mkubwa Ndiye Msaidizi wao, na Yeye ni Mwenye kuwalipiza wale waliowadhulumu na kuwaonea.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net