Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 33

An-Nisaa 4:33

النساء

وَلِكُلٍّ جَعَلْنَا مَوَٰلِىَ مِمَّا تَرَكَ ٱلْوَٰلِدَانِ وَٱلْأَقْرَبُونَ ۚ وَٱلَّذِينَ عَقَدَتْ أَيْمَـٰنُكُمْ فَـَٔاتُوهُمْ نَصِيبَهُمْ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ شَهِيدًا

Maana

Na kila mmoja tumemfanyia warithi katika yale waliyoyaacha wazazi wawili na jamaa. Na wale mliofungamana nao kwa viapo, wapeni fungu lao. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Shahidi juu ya kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na kila mmoja tumemwekea warithi katika waliyo yaacha wazazi wawili na jamaa. Na mlio fungamana nao ahadi wapeni fungu lao. Hakika Mwenyezi Mungu ni Shahidi wa kila kitu. [33]

[33] Na wote, wanaume na wanawake, tumewajaalia kuwa wanastahiki urithi wao wa kuwarithi wazazi wawili, na jamaa, na wale ambao mfiliwa amefungamana nao kwa agano ambalo matokeo yake ni kuwa amrithi ijapokuwa si jamaa, na amsaidie pindi anahitajia msaada kuwa ni badala yake. Basi mpeni haki yake kila mwenye haki, wala msipunguze kitu. Hakika Mwenyezi Mungu anakuangalieni kwa kila kitu, na yuko pamoja nanyi, anashuhudia yote myafanyayo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kila mmoja katika nyinyi tumemwekea warithi wenye kukirithi kilichoachwa na wazazi wawili na jamaa wa karibu. Na wale mliofungamana nao kwa mayamini yaliyotiliwa mkazo kuwa mtanusuriana na mtawapa kitu katika urithi, basi wapeni walichokadiriwa. Kurithiana kwa mikataba ya kunusuriana kulikuwako mwanzo wa Uislamu, kisha hukumu yake ikaondolewa kwa kuteremka aya za mirathi. Hakika Allah Mtukufu ni Mwenye kuona kila kitu katika vitendo vyenu na Atawalipa kulingana navyo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net