An-Nisaa 4:32
النساءوَلَا تَتَمَنَّوْا۟ مَا فَضَّلَ ٱللَّهُ بِهِۦ بَعْضَكُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ ۚ لِّلرِّجَالِ نَصِيبٌ مِّمَّا ٱكْتَسَبُوا۟ ۖ وَلِلنِّسَآءِ نَصِيبٌ مِّمَّا ٱكْتَسَبْنَ ۚ وَسْـَٔلُوا۟ ٱللَّهَ مِن فَضْلِهِۦٓ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ بِكُلِّ شَىْءٍ عَلِيمًا
Wala msitamani alichowafadhilisha kwacho Mwenyezi Mungu baadhi yenu kuliko wengine. Wanaume wana fungu katika walivyovichuma, na wanawake wana fungu katika walivyovichuma. Na mwombeni Mwenyezi Mungu katika fadhila zake. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua kila kitu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wala msitamani alicho wafadhili Mwenyezi Mungu baadhi yenu kuliko wengine. Wanaume wana fungu katika walio vichuma, na wanawake wana fungu katika walio vichuma. Na muombeni Mwenyezi Mungu fadhila zake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu. [32]
[32] Wala haifai wanaume kutamani yale waliyo khusishwa nayo wanawake, wala haiwafalii wanawake kutamani waliyo khusishwa nayo wanaume. Kwani kila kikundi kina sehemu yake kwa mujibu wa tabia ya maumbile ya kazi zinazo wawajibikia, na haki wanazo ongezewa. Basi kila mmoja ajielekeze kutaraji ziada ya fadhila za Mwenyezi Mungu kwa kukuza vipawa alivyo pewa yeye na kutafuta msaada juu ya waajibu ulio juu yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi timamu wa kila kitu, na mtu amepewa namna ya kila kitu kinacho msilihi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wala msiyatamani mambo ambayo Allah Mtukufu Amewafadhilisha kwayo, baadhi yenu juu ya wengine, ya vipewa na riziki na mengineyo. Kwani Allah Mtukufu Amewapa wanaume malipo kulingana na matendo yao na Amewapa wanawake malipo kulingana na matendo yao. Na muombeni Allah Mtukufu Aliye Mkarimu na Mpaji Awape nyongeza za ukarimu Wake, badala ya kutamani tu. Hakika Allah Mtukufu kwa kila kitu ni Mjuzi, na Yeye Anayajua zaidi yanayowafaa waja Wake miongoni mwa kheri Aliyowagawia,
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net