An-Nisaa 4:31
النساءإِن تَجْتَنِبُوا۟ كَبَآئِرَ مَا تُنْهَوْنَ عَنْهُ نُكَفِّرْ عَنكُمْ سَيِّـَٔاتِكُمْ وَنُدْخِلْكُم مُّدْخَلًا كَرِيمًا
Mkiyaepuka makubwa ya yale mnayokatazwa, tutawafutia makosa yenu madogo, na tutawaingiza pahali pa kuingia patukufu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mkiyaepuka makubwa mnayo katazwa, tutakufutieni makosa yenu madogo, na tutakuingizeni mahali patukufu. [31]
[31] Mkiyaachilia mbali madhambi makubwa makubwa anayo kukatazeni Mwenyezi Mungu, tutakusameheni makosa yaliyo duni ya hayo, maadamu mnafanya ukomo wa juhudi yenu kwenda sawa; na tutakuwekeni duniani na Akhera mwahali penye ihsani na hishima kwenu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Mkijiepusha, enyi Waumini, na madhambi makubwa, kama kumshrikisha Allah Mtukufu, kuwaasi wazazi wawili, kumuua mtu bila ya haki na mengineyo, tutawasamehe madhambi yenu madogo yaliyo chini ya hayo na tutawaingiza mahali pema pa kuingia, napo ni Pepo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net