Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 30

An-Nisaa 4:30

النساء

وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ عُدْوَٰنًا وَظُلْمًا فَسَوْفَ نُصْلِيهِ نَارًا ۚ وَكَانَ ذَٰلِكَ عَلَى ٱللَّهِ يَسِيرًا

Maana

Na mwenye kufanya hayo kwa kupita mipaka na udhalimu, basi tutamwingiza motoni. Na hilo ni jepesi kwa Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na mwenye kutenda hayo kwa uadui na udhaalimu, basi huyo tutamwingiza Motoni. Na hilo ni jepesi kwa Mwenyezi Mungu. [30]

[30] Na mwenye kuyatenda aliyo yaharimisha Mwenyezi Mungu kwa uvamizi na kupindukia haki yake, basi tutamtia Motoni ateketee huko. Na hayo ni madogo na mepesi kabisa kwa Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Mwenye kutenda Aliyoyakataza Allah Mtukufu ya kuchukua mali ya haramu, kama kuiba, kunyang’anya na kudanganya, kwa dhuluma na kukiuka mipaka ya Sheria, Allah Mtukufu Atamuingiza kwenye Moto alionje joto lake. Na hilo kwa Allah Mtukufu ni jepesi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net