An-Nisaa 4:29
النساءيَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَا تَأْكُلُوٓا۟ أَمْوَٰلَكُم بَيْنَكُم بِٱلْبَـٰطِلِ إِلَّآ أَن تَكُونَ تِجَـٰرَةً عَن تَرَاضٍ مِّنكُمْ ۚ وَلَا تَقْتُلُوٓا۟ أَنفُسَكُمْ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ بِكُمْ رَحِيمًا
Enyi mlioamini! Msizile mali zenu baina yenu kwa batili, isipokuwa ikiwa ni biashara kwa kuridhiana wenyewe. Wala msijiue. Hakika, Mwenyezi Mungu kwenu ni Mrehemevu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Enyi mlio amini! Msiliane mali yenu kwa dhulma, isipo kuwa iwe biashara kwa kuridhiana wenyewe. Wala msijiuwe. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwarehemuni. [29]
[29] Enyi mlio amini! Msinyang'anyane mali nyinyi kwa nyinyi. Lakini ipo ruhusa kufanya biashara kwa kuridhiana. Wala msijiteketeze kwa kuacha amri za Mola wenu Mlezi. Wala mmoja wenu asimtende uwovu mwenziwe, kwani nyote ni nafsi moja. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye rehema daima kwenu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Enyi mliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkafuata sheria Yake kivitendo! Si halali kwa baadhi yenu kula mali ya wengine kati yenu pasi na haki, isipokuwa ikiwa itaambatana na Sheria na chumo la halali litokanalo na kuridhiana baina yenu. Na wala msiuane nyinyi kwa nyinyi mkaziangamiza nafsi zenu kwa kufanya maasia yaliyoharamishwa na Allah Mtukufu. Hakika Allah Mtukufu ni Mwenye huruma sana katika kila Alilowaamrisha kwalo na kuwakataza nalo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net