Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 28

An-Nisaa 4:28

النساء

يُرِيدُ ٱللَّهُ أَن يُخَفِّفَ عَنكُمْ ۚ وَخُلِقَ ٱلْإِنسَـٰنُ ضَعِيفًا

Maana

Na Mwenyezi Mungu anataka kwamba awahafifishie, na mwanadamu ameumbwa dhaifu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mwenyezi Mungu anataka kukupunguzieni taabu, na mwanaadamu ameumbwa dhaifu. [28]

[28] Mwenyezi Mungu anataka kukufanyieni wepesi katika kutunga sharia ambazo ndani yake zina sahala na takhfifu kwenu. Kwani hakika Mwenyezi Mungu amemuumba mwanaadamu kiumbe dhaifu katika kupambana na matamanio na maelekeo ya nafsi. Kwa hivyo yanayo mlazimu katika sharia yana wepesi na wasaa. Na hayo kwa fadhila yake na taisiri yake Mwenyezi Mungu ndiyo anayo walazimisha waja wake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu, Aliyetukuka, kwa sheria Zake Alizowaekea, Anataka kuwafanyia sahali na kutowafanyia mkazo, kwa kuwa nyinyi mumeumbwa mkiwa madhaifu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net