Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 27

An-Nisaa 4:27

النساء

وَٱللَّهُ يُرِيدُ أَن يَتُوبَ عَلَيْكُمْ وَيُرِيدُ ٱلَّذِينَ يَتَّبِعُونَ ٱلشَّهَوَٰتِ أَن تَمِيلُوا۟ مَيْلًا عَظِيمًا

Maana

Na Mwenyezi Mungu anataka kuwakubalia toba zenu, na wale wanaofuata matamanio wanataka kwamba mjipinde kujipinda kukubwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Mwenyezi Mungu anataka kukurejezeni kwenye ut'iifu wake, na wanao taka kufuata matamanio wanataka mkengeuke makengeuko makubwa. [27]

[27] Na Mwenyezi Mungu anataka mrejee katika ut'iifu wake, na wale wanao fuata ladha zao, na matamanio yao machafu, miongoni mwa makafiri na waasi, wanataka muwe mbali kabisa na njia ya haki.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Allah Mtukufu Anataka kuwakubalia toba zenu na kuyasamehe makosa yenu; na wale wanaofuata matamanio yao na starehe zao, wanataka mupotoke muwe kando na Dini kabisa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net