Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 26

An-Nisaa 4:26

النساء

يُرِيدُ ٱللَّهُ لِيُبَيِّنَ لَكُمْ وَيَهْدِيَكُمْ سُنَنَ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ وَيَتُوبَ عَلَيْكُمْ ۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ

Maana

Mwenyezi Mungu anataka kwamba awabainishie, na awaongoze nyendo za wale waliokuwa kabla yenu, na akubali toba zenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye hekima.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mwenyezi Mungu anataka kukubainishieni na kukuongozeni nyendo za walio kuwa kabla yenu, na akurejezeni kwenye ut'iifu wake. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye hikima. [26]

[26] Mwenyezi Mungu anataka kukuwekeeni wazi njia yenye maslaha kabisa, na akuongoeni kwenye nyendo njema za walio kuwa kabla yenu, na akurejesheni kwenye njia ya ut'iifu wake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyajua vyema mambo yenu, ni Mwenye kupanga baraabara katika hukumu zake kwa yanayo silihi mambo yenu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Katika kuwaekea Sheria hizi, Allah Mtukufu Anataka kuwafunulia wazi alama za dini Yake iliyolingana na hukumu Zake zenye hekima, kuwaonesha njia za Mitume na watu wema waliokuwa kabla yenu katika halali na haramu na kuwakubalia toba zenu kwa kuwarudisha kwenye kumtii Allah Mtukufu. Na Yeye, Aliyetakasika na sifa pungufu, ni Mjuzi wa yale yenye kutengeneza mambo ya waja Wake, ni Mwenye hekima katika sheria Zake Alizowaekea.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net