Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 25

An-Nisaa 4:25

النساء

وَمَن لَّمْ يَسْتَطِعْ مِنكُمْ طَوْلًا أَن يَنكِحَ ٱلْمُحْصَنَـٰتِ ٱلْمُؤْمِنَـٰتِ فَمِن مَّا مَلَكَتْ أَيْمَـٰنُكُم مِّن فَتَيَـٰتِكُمُ ٱلْمُؤْمِنَـٰتِ ۚ وَٱللَّهُ أَعْلَمُ بِإِيمَـٰنِكُم ۚ بَعْضُكُم مِّنۢ بَعْضٍ ۚ فَٱنكِحُوهُنَّ بِإِذْنِ أَهْلِهِنَّ وَءَاتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ بِٱلْمَعْرُوفِ مُحْصَنَـٰتٍ غَيْرَ مُسَـٰفِحَـٰتٍ وَلَا مُتَّخِذَٰتِ أَخْدَانٍ ۚ فَإِذَآ أُحْصِنَّ فَإِنْ أَتَيْنَ بِفَـٰحِشَةٍ فَعَلَيْهِنَّ نِصْفُ مَا عَلَى ٱلْمُحْصَنَـٰتِ مِنَ ٱلْعَذَابِ ۚ ذَٰلِكَ لِمَنْ خَشِىَ ٱلْعَنَتَ مِنكُمْ ۚ وَأَن تَصْبِرُوا۟ خَيْرٌ لَّكُمْ ۗ وَٱللَّهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

Maana

Na asiyeweza kati yenu kupata mali ya kuolea wanawake wa kiungwana Waumini, basi na aoe katika vijakazi Waumini iliowamiliki mikono yenu ya kulia. Na Mwenyezi Mungu anajua vyema imani yenu. Nyinyi mmetokana wenyewe kwa wenyewe. Basi waoeni kwa idhini ya watu wao, na wapeni mahari yao kulingana na ada, wawe wanawake wema, si makahaba wala si mahawara. Na wanapoolewa kisha wakafanya uchafu, basi adhabu yao itakuwa ni nusu ya adhabu waliyowekewa waungwana. Hayo ni kwa yule miongoni mwenu anayeogopa kuingia katika zinaa. Na mkisubiri, ndiyo bora kwenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta dhambi, Mwenye kurehemu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na asiyeweza kati yenu kupata mali ya kuolea wanawake wa kiungwana Waumini, na aoe katika vijakazi Waumini iliyo wamiliki mikono yenu ya kulia. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa imani yenu. Nyinyi mmetokana wenyewe kwa wenyewe. Basi waoeni kwa idhini ya watu wao, na wapeni mahari yao kama ada, wawe wanawake wema, si makahaba wala si mahawara. Na wanapo olewa kisha wakafanya uchafu basi adhabu yao itakuwa ni nusu ya adhabu waliyo wekewa waungwana. Hayo ni kwa yule miongoni mwenu anaye ogopa kuingia katika zina. Na mkisubiri ndio bora kwenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe na Mwenye kurehemu. [25]

[25] Asiye weza kati yenu kuwaoa wanawake Waumini wa kiungwana basi na aowe anaye muweza katika wanawake Waumini walio milikiwa. Na Mwenyezi Mungu anajua vyema ukweli wa Imani yenu na ikhlasi yenu. Wala msione uvunjifu kuwaowa hao vijakazi, kwani nyinyi na wao ni sawa katika Dini. Basi waoweni kwa idhini ya watu wao, na muwape mahari yao mliyo wakadiria kwa mujibu ya ilivyo zowewa kati yenu kwa ajili ya kutendeana mema na kutimiza haki. Na chagueni wanawake walio safi, msichague wazinifu kwa dhaahiri wala mahawara wa kinyumba. Na hao wakija zini baada ya kuolewa basi adabu yao ni nusu ya muungwana. Na huku kuhalalishiwa kuowa wajakazi mnapo kuwa hamuwezi kunajuzu kwa anaye ogopa taabu zinazo pelekea zina. Na mkisubiri kuto owa wajakazi na mkakaa safi ni bora kwenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira, na Mkubwa wa kurehemu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na asiyeweza kujimudu mahari ya Waumini waungwana, basi ni hiyari yake aoe wengineo miongoni mwa wanawake wenu waumini waliomilikiwa. Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Ndiye Mjuzi wa ukweli wa Imani yenu. Baadhi yenu mnatokana na wengine katika nyinyi. Basi waoeni kwa ruhusa ya watu wao, na wapeni mahari yao mliokubaliana nayo kwa moyo wenu safi, na wawe ni wenye kujiepusha na haramu, si wenye kudhihirisha zina, wala si wenye kuzini kwa siri kwa kufanya urafiki na wanaume. Wakiolewa na wakafanya kitendo kichafu cha kuzini, adhabu yao ni kadiri ya nusu ya adhabu ya walio huru. Huyo aliyeruhusiwa kuoa wajakazi wenye sifa zilizotajwa, ameruhusiwa iwapo anachelea kuingia kwenye uzinifu na ikawa ni uzito kwake kuvumilia kujizuia. Na kuvumilia kutooa wajakazi pamoja na kujihifadhi ni aula na bora zaidi. Allah Mtukufu, Aliyetukuka, ni Mwingi wa msamaha kwenu, ni Mwenye kuwahurumia sana kwa kuwaruhusu muwaoe wao(hao wajakazi) mkishindwa kuwaoa waungwana.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net