An-Nisaa 4:24
النساءوَٱلْمُحْصَنَـٰتُ مِنَ ٱلنِّسَآءِ إِلَّا مَا مَلَكَتْ أَيْمَـٰنُكُمْ ۖ كِتَـٰبَ ٱللَّهِ عَلَيْكُمْ ۚ وَأُحِلَّ لَكُم مَّا وَرَآءَ ذَٰلِكُمْ أَن تَبْتَغُوا۟ بِأَمْوَٰلِكُم مُّحْصِنِينَ غَيْرَ مُسَـٰفِحِينَ ۚ فَمَا ٱسْتَمْتَعْتُم بِهِۦ مِنْهُنَّ فَـَٔاتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ فَرِيضَةً ۚ وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِيمَا تَرَٰضَيْتُم بِهِۦ مِنۢ بَعْدِ ٱلْفَرِيضَةِ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمًا
Na wanawake wenye waume, isipokuwa waliomilikiwa na mikono yenu ya kulia. Ndiyo sheria ya Mwenyezi Mungu juu yenu. Na mmehalalishiwa wasiokuwa hao, mtafute kwa mali zenu kwa kuoa pasi na kuzini. Kama mnavyostarehe nao, basi wapeni mahari yao kwa kuwa ni wajibu. Wala hakuna ubaya juu yenu kwa mtakachokubaliana baada ya kutimiza wajibu. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye hekima.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
NA WANAWAKE wenye waume, isipo kuwa walio milikiwa na mikono yenu ya kulia. Ndiyo Sharia ya Mwenyezi Mungu juu yenu. Na mmehalilishiwa wasio kuwa hao, mtafute kwa mali yenu kwa kuowa pasina kuzini. Kama mnavyo starehe nao, basi wapeni mahari yao kwa kuwa ni waajibu. Wala hapana lawama juu yenu kwa mtakacho kubaliana baada ya kutimiza waajibu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua na Mwenye hikima. [24]
[24] Haramu kwenu kuoa wake za watu wote, waungwana na wasio waungwana, ila mateka mlio wateka katika vita baina yenu na makafiri. Kwani ndoa zao zilizo pita zinafutika kwa kutekwa. Wanakuwa halali kwenu baada ya kuhakikisha hawana mimba. Basi shikeni aliyo kuandikieni Mwenyezi Mungu kuhishimu mlicho katazwa. Isipo kuwa hao wanawake Waumini walio maharimu yenu, mwaweza kutafuta wanawake mkawaoa kwa mali yenu, bila ya kuzini au kuweka kinyumba. Kila mwanamke mliye starehe naye baada ya kumwoa mpeni mahari yake kama mlivyo patana. Hapana ubaya kwenu ikiwa watakuridhieni kupunguza au kuongeza. Mwenyezi Mungu daima anayaangalia mambo ya waja wake, na ni mwenye kuwapangia hukumu zinazo wasilihi kwa maisha yao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na ni haramu kwenu kuwaoa wanawake walioolewa, isipokuwa wale mliowateka katika jihadi. Hao ni halali kwenu kuwaoa baada ya kutakasika vizazi vyao kwa kipindi kimoja cha hedhi. Allah Mtukufu Amewaandikia uharamu wa kuwaoa hao, na Amewaruhusu kuwaoa wengineo, miongoni mwa wale Aliowahalalishia kuwataka kwa ndoa mkitumia pesa zenu kujihifadhi msitende haramu. Basi wale mliostarehe nao, miongoni mwao, kwa ndoa sahihi, wapeni mahari yao ambayo ni haki yao iliyolazimishwa na Allah Mtukufu juu yenu. Na si makosa kwenu, kwa makubaliano yaliyofikiwa baina yenu kwa kuridhiana, kupunguza au kuongeza kiwango cha mahari baada ya kuamuliwa kiwango chake. Allah Mtukufu ni Mjuzi wa mambo ya waja Wake, ni Mwenye hekima katika hukumu zake na uendeshaji Wake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net