An-Nisaa 4:45
النساءوَٱللَّهُ أَعْلَمُ بِأَعْدَآئِكُمْ ۚ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ وَلِيًّا وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ نَصِيرًا
Na Mwenyezi Mungu anawajua vyema maadui zenu. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Mlinzi, na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Mwenye kunusuru.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Mwenyezi Mungu anawajua vyema maadui zenu. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa ni Mlinzi, na anatosha kuwa ni Mwenye kukunusuruni. [45]
[45] Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi zaidi kuliko nyinyi kuwajua maadui zenu wa kweli, na anatambua zaidi yaliyo ndani ya nafsi zao. Ulinzi wa Mwenyezi Mungu unakulindeni, na unakuangalieni, na unakutosheni. Basi msitafute ulinzi wa mwenginewe usio kuwa wake. Msaada na nusura yake inakutoshelezeni; basi msiwe kutaka msaada wa mwenginewe.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Allah Mtukufu, Aliyetakasika na sifa pungufu na kutukuka, Anaujua zaidi kuliko nyinyi, enyi Waumini, uadui wa hawa Mayahudi juu yenu. Na inatosha kuwa Allah Mtukufu Ndiye Msimamizi wa kuwasimamia, na inatosha kuwa Yeye Ndiye Mnusuru wa kuwanusuru juu ya maadui zenu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net