Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 20

An-Nisaa 4:20

النساء

وَإِنْ أَرَدتُّمُ ٱسْتِبْدَالَ زَوْجٍ مَّكَانَ زَوْجٍ وَءَاتَيْتُمْ إِحْدَىٰهُنَّ قِنطَارًا فَلَا تَأْخُذُوا۟ مِنْهُ شَيْـًٔا ۚ أَتَأْخُذُونَهُۥ بُهْتَـٰنًا وَإِثْمًا مُّبِينًا

Maana

Na mkitaka kubadilisha mke pahali pa mke hali ya kuwa mmempa mmoja wao chungu ya mali, basi msichukue katika hiyo kitu chochote. Je, mnaichukua kwa dhuluma na kosa lililo wazi?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na mkitaka kubadilisha mke mahali pa mke, na hali mmoja wao mmempa chungu ya mali, basi msichukue katika hayo kitu chochote. Je, mtachukua kwa dhulma na kosa lilio wazi? [20]

[20] Na pindi ikiwa mnataka kubadili mke pahala pa mke mwengine, na ikawa mmempa mmoja wao mali mengi basi si halali kwenu kuchukua chochote katika hayo. Jee mtachukua hayo kwa njia ya upotovu na kwa dhambi iliyo wazi?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na mnapotaka kubadilisha mke mahali pa mke mwengine, na mkawa mumempa yule mnayetaka kumtaliki mali mengi yakiwa ni mahari yake. Si halali kwenu kuchukua chochote katika mali hayo. Je mnayachukua kwa njia ya urongo na uzushi ulio wazi?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net