Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 19

An-Nisaa 4:19

النساء

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَا يَحِلُّ لَكُمْ أَن تَرِثُوا۟ ٱلنِّسَآءَ كَرْهًا ۖ وَلَا تَعْضُلُوهُنَّ لِتَذْهَبُوا۟ بِبَعْضِ مَآ ءَاتَيْتُمُوهُنَّ إِلَّآ أَن يَأْتِينَ بِفَـٰحِشَةٍ مُّبَيِّنَةٍ ۚ وَعَاشِرُوهُنَّ بِٱلْمَعْرُوفِ ۚ فَإِن كَرِهْتُمُوهُنَّ فَعَسَىٰٓ أَن تَكْرَهُوا۟ شَيْـًٔا وَيَجْعَلَ ٱللَّهُ فِيهِ خَيْرًا كَثِيرًا

Maana

Enyi mlioamini! Si halali kwenu kuwarithi wanawake kwa nguvu. Wala msiwadhikishe ili muwapokonye baadhi ya mlivyowapa, isipokuwa wakifanya uchafu ulio wazi. Na kaeni nao kwa wema. Na ikiwa mmewachukia, basi huenda mkakichukia kitu, na Mwenyezi Mungu ametia heri nyingi ndani yake.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi mlio amini! Si halali kwenu kuwarithi wanawake kwa nguvu. Wala msiwadhikishe ili mwapokonye baadhi ya mlivyo wapa - isipo kuwa wakifanya uchafu ulio wazi. Na kaeni nao kwa wema, na ikiwa mmewachukia, basi huenda mkakichukia kitu, na Mwenyezi Mungu ametia kheri nyingi ndani yake. [19]

[19] Enyi mlio amini! Haikujuziini kuwafanya wanawake kama bidhaa, mkiwarithi wake zenu bila ya mahari na bila ya ridhaa yao. Wala msiwadhulumu kwa kuwadhikisha ili wapate kusamehe baadhi ya mahari mlio wapa. Wala msiwadhiki ili wapate kukurejesheeni mali mlio wapa, ila ikiwa wakifanya kosa wazi la kuwacha ut'iifu, au la tabia mbovu, au la ukahaba. Hapo mnaweza kuwadhikisha au kuchukua baadhi ya mlicho wapa wakati wa kufarikiana nao. Na ni waajibu wenu, enyi Waumini, kukaa na wake zenu kwa vizuri, kwa maneno mema na vitendo vyema. Ikiwa mtawachukia kwa aibu fulani katika tabia au katika umbo au mengineyo, basi juu ya hivyo subirini. Msifanye haraka kuwaacha, kwani asaa Mwenyezi Mungu akajaalia kheri nyingi katika hicho hicho mkichukiacho. Na ujuzi wa mambo yote uko kwa Mwenyezi Mungu tu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi mlioamini, haifai kwenu kuwafanya wake wa baba zenu ni miongoni mwa mali yalioachwa kurithiwa, mkawa mnafanya mtakavyo kwao: kwa kuwaoa, kuwakataza wasiolewe au kuwaoza waume wengine, hali ya kuwa wao hawayataki hayo yote. Na pia haifai kwenu kuwadhuru wake zenu kwa kuwa mnawachukia, ili wapate kusamehe baadhi ya mlivyowapa, mahari au vinginevyo. Isipokuwa wakiwa wamefanya jambo ovu, kama uzinifu, hapo mnayo nafasi ya kuwazuia mpaka mkitwae mlichowapa. Na kule kukaa kwenu na wake zenu yatakikana kuwe ni juu ya misingi ya heshima na mapenzi na kuwatekelezea haki zao. Na iwapo mtawachukia kwa sababu yoyote katika sababu za kidunia, basi kuweni na subira. Kwani huenda mkachukia jambo, miongoni mwa mambo, na ikawa ndani yake muna kheri nyingi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net