An-Nisaa 4:18
النساءوَلَيْسَتِ ٱلتَّوْبَةُ لِلَّذِينَ يَعْمَلُونَ ٱلسَّيِّـَٔاتِ حَتَّىٰٓ إِذَا حَضَرَ أَحَدَهُمُ ٱلْمَوْتُ قَالَ إِنِّى تُبْتُ ٱلْـَٔـٰنَ وَلَا ٱلَّذِينَ يَمُوتُونَ وَهُمْ كُفَّارٌ ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ أَعْتَدْنَا لَهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا
Wala hawana toba wale wafanyao maovu mpaka yakamfikia mmoja wao mauti, kisha hapo akasema: Hakika, mimi sasa nimetubu. Wala wale wanaokufa hali ya kuwa wao ni makafiri. Hao tumewaandalia adhabu chungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wala hawana toba wale wafanyao maovu mpaka yakamfikia mmoja wao mauti, kisha hapo akasema: Hakika mimi sasa nimetubia. Wala wale wanao kufa na hali wao ni makafiri. Hao tumewaandalia adhabu chungu. [18]
[18] Toba isiyo kubaliwa ni ya wanao fanya maasi kisha hawafanyi haraka kuyajutia mpaka mmoja afikwapo na mauti. Tena hapo husema: Sasa mimi natangaza majuto na toba. Kadhaalika toba haikubaliwi kutokana na wanao kufa katika ukafiri. Mwenyezi Mungu ameyaandalia makundi mawili hayo adhabu ya kutia uchungu huko kwenye nyumba ya malipo, Akhera.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kukubaliwa toba si kwa wale wanaoendelea kufanya maasia bila ya kurudi kwa Mola wao mpaka wakafikiwa na shida ya mauti, hapo mmoja wao aseme, «Mimi sasa nimetubia.» Kama ambavyo haikubaliwi toba ya wale wanaokufa na hali wao ni wenye kukanusha, ni wenye kupinga upweke wa Allah Mtukufu na ujumbe wa Mtume Wake Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie. Hao wenye kuendeleza maasia hadi kufa kwao, na wakanushaji ambao wanakufa na huku ni makafiri, tumewatayarishia adhabu iumizayo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net