An-Nisaa 4:17
النساءإِنَّمَا ٱلتَّوْبَةُ عَلَى ٱللَّهِ لِلَّذِينَ يَعْمَلُونَ ٱلسُّوٓءَ بِجَهَـٰلَةٍ ثُمَّ يَتُوبُونَ مِن قَرِيبٍ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ يَتُوبُ ٱللَّهُ عَلَيْهِمْ ۗ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلِيمًا حَكِيمًا
Hakika, toba inayokubaliwa na Mwenyezi Mungu ni ya wale wafanyao uovu kwa ujinga, kisha wakatubia kwa haraka. Hao ndio Mwenyezi Mungu huwakubalia toba yao, na Mwenyezi Mungu ni mwenye kujua, Mwenye hekima.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika toba inayo kubaliwa na Mwenyezi Mungu ni ya wale wafanyao uovu kwa ujinga, kisha wakatubia kwa haraka. Hao ndio Mwenyezi Mungu huwakubalia toba yao, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na ni Mwenye hikima. [17]
[17] Hakika toba imedhaminiwa na Mwenyezi Mungu kwa watendao maovu katika hali ya ujinga, na kupitikiwa na kutoangalia vyema, kisha wakafanya haraka ya kutubu kabla ya kufikiwa na mauti. Hawa basi Mwenyezi Mungu anaikubali toba yao, naye ni Mjuzi, haumfichikii ukweli wa toba, ni Mwenye hikima, hakosei katika kupima.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwa kweli, Allah Mtukufu Anaikubali toba itokayo kwa wale wanaofanya maasia na madhambi kwa ujinga wao wa kutojua ubaya wake na kwamba yanasababisha hasira za Allah Mtukufu.- Kwa hivyo, kila anayemuasi Allah Mtukufu, kwa kukosea au kwa kusudi, yeye ni mjinga kwa kuzingatia maana haya, hata kama anajua kuwa ni haramu.- kisha, hao wanaokubaliwa toba zao, wakarudi kwa Mola wao kwa majuto na kutii kabla ya kukabiliwa na mauti. Basi hao ndio wale ambao Allah Mtukufu Anaikubali toba yao. Na Allah Mtukufu daima ni Mjuzi kwa viumbe Wake, ni Mwingi wa hekima katika uendeshaji Wake mambo na makadirio Yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net