An-Nisaa 4:21
النساءوَكَيْفَ تَأْخُذُونَهُۥ وَقَدْ أَفْضَىٰ بَعْضُكُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ وَأَخَذْنَ مِنكُم مِّيثَـٰقًا غَلِيظًا
Na vipi mnaichukua ilhali mlikwishaingiliana nyinyi kwa nyinyi, nao (wanawake) walikwishachukua kutoka kwenu agano lililo madhubuti?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na mtachukuaje na ilhali mmekwisha ingiliana nyinyi kwa nyinyi, na wao wanawake wamechukua kwenu ahadi iliyo madhubuti? [21]
[21] Na vipi ikufalieni nyinyi kutaka kurudishiwa mahari mliyo kwisha yatoa, na hali mlikwisha changanyika nyinyi kwa nyinyi, na wao wanawake wakafungamana nanyi kwa agano lenye nguvu ambalo kwalo Mwenyezi Mungu amewajibisha muingiane nao kwa ndoa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na vipi itakuwa ni halali kwenu kukichukua mlichowapa cha mahari, na kila mmoja kati yenu amejiliwaza na mwenzake kwa kuingiliana na walichukua kutoka kwenu ahadi iliyo nzito ya kuwa mtashikamana nao kwa wema au mtaepukana nao kwa ihsani?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net