Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 142

An-Nisaa 4:142

النساء

إِنَّ ٱلْمُنَـٰفِقِينَ يُخَـٰدِعُونَ ٱللَّهَ وَهُوَ خَـٰدِعُهُمْ وَإِذَا قَامُوٓا۟ إِلَى ٱلصَّلَوٰةِ قَامُوا۟ كُسَالَىٰ يُرَآءُونَ ٱلنَّاسَ وَلَا يَذْكُرُونَ ٱللَّهَ إِلَّا قَلِيلًا

Maana

Hakika wanafiki wanamhadaa Mwenyezi Mungu, na hali ni Yeye ndiye mwenye kuwahadaa wao. Na wanapoinuka kusali huinuka kwa unyong'onyo, wanajionyesha kwa watu tu, wala hawamdhukuru Mwenyezi Mungu ila kidogo tu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika wanaafiki wanamkhadaa Mwenyezi Mungu, na hali ni Yeye ndiye mwenye kuwakhadaa wao. Na wanapo inuka kuswali huinuka kwa unyong'onyo, wanajionyesha kwa watu tu, wala hawamdhukuru Mwenyezi Mungu ila kidogo tu. [142]

[142] Hakika wanaafiki, kwa ule unaafiki wao, wanadhani kuwa wanamkhadaa Mwenyezi Mungu Mtukufu na wanamficha hakika ya nafsi zao. Na Mwenyezi Mungu Subhanahu ni Yeye ndiye anaye wakhadaa wao. Basi Yeye huwapururia kuwapa muhula, na anawawacha mpaka wabobee katika maovu yao, kisha ndio awahisabu kwa waliyo yatenda. Na hawa wanaafiki wana dhaahiri ya kuonekana, na ya ndani ya nafsi zao. Yale ya kuonekana ni vile kuwa wakiinuka kwenda kuswali huinuka kwa uvivu, kwa unyong'onyo. Na Swala yao ni riya tu, kuonyesha, si ya kweli. Na ya ndani ni kuwa hawakumbuki kumtaja Mwenyezi Mungu ila kwa nadra, kwa tukizi. Na lau kuwa wanamkumbuka vilivyo wangeli uacha unaafiki

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika mbinu ya wanafiki hawa ni kumhadaa Allah Mtukufu kwa Imani wanaojionyesha nayo na ukafiri wanaouficha, kwa kudhani kuwa mbinu yao itafichamana kwa Allah Mtukufu, na hali ni kwamba Allah Mtukufu Ndiye Anayewahadaa na ni Mwenye kuwalipa malipo yanayofanana na vitendo vyao. Wanafiki hawa wanaposimama kutekeleza Swala, wanasimama kufanya hivyo kwa uvivu, wanakusudia, kwa kuswali kwao, kuonekana na kusikika. Na wao hawamtaji Allah Mtukufu, Aliyetukuka, isipokuwa kumtaja kwa uchache.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net