Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 141

An-Nisaa 4:141

النساء

ٱلَّذِينَ يَتَرَبَّصُونَ بِكُمْ فَإِن كَانَ لَكُمْ فَتْحٌ مِّنَ ٱللَّهِ قَالُوٓا۟ أَلَمْ نَكُن مَّعَكُمْ وَإِن كَانَ لِلْكَـٰفِرِينَ نَصِيبٌ قَالُوٓا۟ أَلَمْ نَسْتَحْوِذْ عَلَيْكُمْ وَنَمْنَعْكُم مِّنَ ٱلْمُؤْمِنِينَ ۚ فَٱللَّهُ يَحْكُمُ بَيْنَكُمْ يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ ۗ وَلَن يَجْعَلَ ٱللَّهُ لِلْكَـٰفِرِينَ عَلَى ٱلْمُؤْمِنِينَ سَبِيلًا

Maana

Wale ambao wanawangojelea. Basi mkipata ushindi unaotoka kwa Mwenyezi Mungu, wao husema: "Kwani hatukuwa pamoja nanyi?" Na ikiwa ni sehemu ya makafiri kushinda, wao huwaambia: "Hatukuwa ni waweza wa kukushindeni, nasi tukawakinga kutokana na hawa Waumini?" Basi Mwenyezi Mungu atahukumu baina yenu Siku ya Kiyama, wala Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wale ambao wanakungojeeni, mkipata ushindi unao toka kwa Mwenyezi Mungu wao husema: Si tulikuwa pamoja nanyi vile? Na ikiwa ni sehemu ya makafiri kushinda wao huwaambia: Hatukuwa ni waweza wa kukushindeni, nasi tukakukingeni na hawa Waumini? Basi Mwenyezi Mungu atahukumu baina yenu Siku ya Kiyama, wala Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini. [141]

[141] Mtindo wa wanaafiki ni kukungojeeni kama anavyo ngojea mwenye husda na maya anaye tamani mpate masaibu mnapo kuwa katika vita na maadui. Mkishinda kwa nusra ya Mwenyezi Mungu, na mkafungukiwa njia ya Haki, wao huwaambia Waumini - na hali wao ule ushindi walio pewa wenye Imani na Mwenyezi Mungu umewashtusha : Sisi hatukuwa nanyi? Kwa maana sisi ni jamaa zenu! Na ikiwa ni zamu ya makafiri kupata ushindi, basi wao huwaendea na kuwaambia: Sisi hatukuyashughulikia mambo yenu hata yakawa ni yetu? Na hatukukupeni mapenzi yetu, na tukakulindeni na hawa Waumini? (yaani sisi ni wenzenu). Na Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taa'la atakuhukumuni baina yenu na hawa wanaafiki Siku ya Kiyama. Wala Mwenyezi Mungu hatowapa makafiri njia kuwashinda Waumini maadamu Waumini watashikamana na sifa ya Imani ya kweli na vitendo vyema.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wanafiki ndio wale wanaongojea yatakayowashukia nyinyi, enyi Waumini, ya misukosuko na vita. Iwapo Allah Mtukufu Amewaneemesha kwa fadhila Zake, Akawanusuru juu ya adui yenu na mkapata ngawira, wao wanasema, «Kwani hatukuwa na nyinyi tukiwasaidia?» Na iwapo wakanushaji wa Dini hii wamepata sehemu ya ushindi na ngawira, wao wanasema kuwaambia, «Kwani hatukuwasaidia nyinyi kwa kile tulichowapatia na kuwahami dhidi ya Waumini?» Basi Allah Mtukufu Ataamua baina yao na nyinyi Siku ya Kiyama. Na Allah Mtukufu Hatawapa makafiri njia ya kuwashinda waja Wake wema. Basi mwisho mwema ni wa wacha Mungu, duniani na Akhera.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net