Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 140

An-Nisaa 4:140

النساء

وَقَدْ نَزَّلَ عَلَيْكُمْ فِى ٱلْكِتَـٰبِ أَنْ إِذَا سَمِعْتُمْ ءَايَـٰتِ ٱللَّهِ يُكْفَرُ بِهَا وَيُسْتَهْزَأُ بِهَا فَلَا تَقْعُدُوا۟ مَعَهُمْ حَتَّىٰ يَخُوضُوا۟ فِى حَدِيثٍ غَيْرِهِۦٓ ۚ إِنَّكُمْ إِذًا مِّثْلُهُمْ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ جَامِعُ ٱلْمُنَـٰفِقِينَ وَٱلْكَـٰفِرِينَ فِى جَهَنَّمَ جَمِيعًا

Maana

Naye amekwishawateremshia katika Kitabu hiki ya kwamba mnaposikia Aya za Mwenyezi Mungu zinakanushwa na zinafanyiwa kejeli, basi msikae pamoja nao, mpaka waingie katika mazungumzo mengine. Hivyo mtakuwa nanyi mfano wao hao. Hakika Mwenyezi Mungu atawakusanya wanafiki na makafiri wote pamoja katika Jahannam.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Naye amekwisha kuteremshieni katika Kitabu hiki ya kwamba mnapo sikia Aya za Mwenyezi Mungu zinakanushwa na zinafanyiwa kejeli, basi msikae pamoja nao, mpaka waingie katika mazungumzo mengine. Hivyo mtakuwa nanyi mfano wao hao. Hakika Mwenyezi Mungu atawakusanya wanaafiki na makafiri wote pamoja katika Jahannamu. [140]

[140] Mwenyezi Mungu amekwisha kuteremshieni katika Qur'ani Tukufu kwamba kila mkisikia Aya za Kitabu nyinyi mnaamini, na makafiri wanapinga na wanakejeli. Na ikiwa hivyo ndiyo hali ya makafiri na wanaafiki, na mkasikia kejeli zao, basi msikae nao, mpaka waingie katika mazungumzo mengine waache dhihaki zao. Na nyinyi ikiwa hamtofanya hivyo, mkawa mnasikiliza kejeli zao, basi mtakuwa nanyi kama wao katika kuifanyia maskhara Qur'ani. Mwisho wa makafiri na wanaafiki ni muovu mno, kwani Mwenyezi Mungu atawakusanya wote hao katika Moto wa Siku ya Kiyama.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mola wenu Amewateremshia, enyi Waumini, katika Kitabu Chake kwamba mkisikia aya za Allah Mtukufu zinakanushwa na zinafanyiwa shere, basi msikae pamoja na wakanushaji hao wanaofanya shere, isipokuwa wakiingia kwenye mazungumzo yasiokuwa mazungumzo ya kukanusha na kuzifanyia shere aya za Allah Mtukufu. Nyinyi mkikaa nao, na wao wako katika hali hiyo, mtakuwa ni kama wao, kwa kuwa nyinyi mmeridhika na ukafiri wao na uchezaji shere wao. Na mwenye kuridhika na maasia ni kama mwenye kuyafanya. Hakika Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Atawakusanya wanafiki na makafiri wote ndani ya Moto wa Jahanamu ambapo humo watakumbana na ukali wa adhabu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net