Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 139

An-Nisaa 4:139

النساء

ٱلَّذِينَ يَتَّخِذُونَ ٱلْكَـٰفِرِينَ أَوْلِيَآءَ مِن دُونِ ٱلْمُؤْمِنِينَ ۚ أَيَبْتَغُونَ عِندَهُمُ ٱلْعِزَّةَ فَإِنَّ ٱلْعِزَّةَ لِلَّهِ جَمِيعًا

Maana

Wale ambao huwafanya makafiri kuwa ndio marafiki wandani badala ya Waumini. Je, wanataka wapate kwao utukufu? Basi hakika utukufu wote ni wa Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wale ambao huwafanya makafiri kuwa ndio marafiki badala ya Waumini. Je! Wanataka wapate kwao utukufu? Basi hakika utukufu wote ni wa Mwenyezi Mungu. [139]

[139] Hao wanaafiki huufanya utawala wa makafiri uwe juu yao, na wanawawacha Waumini. Basi hebu hivyo wanataka wapate utukufu kwa hawa makafiri? Hakika utukufu uko kwa Mwenyezi Mungu peke yake. Yeye huwapa waja wake wenye kuamini. Na mwenye kutaka utukufu kwa Mwenyezi Mungu atatukuka, na mwenye kutaka utukufu kwa mwenginewe atadhalilika.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ambao wanawategemea makafiri na kuwafanya ni wasaidizi wao, na wanaacha kuwapenda Waumini na kuwategemea, wala hawana haja ya mapenzi yao. Kwani wanatafuta, kwa hilo kuokolewa na kupata hifadhi kwa makafiri? Hili wao hawalimiliki. Kwani uokozi, enzi na nguvu, vyote ni vya Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Peke Yake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net