An-Nisaa 4:138
النساءبَشِّرِ ٱلْمُنَـٰفِقِينَ بِأَنَّ لَهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا
Wabashirie wanafiki kwamba hakika wana adhabu chungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wabashirie wanaafiki kwamba watapata adhabu chungu,. [138]
[138] Ewe Mtume Mtukufu! Waonye wanaafiki kwamba Siku ya Kiyama watapata adhabu chungu yenye kuumiza.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wape bishara, ewe Mtume, wanafiki - nao ni wale wanaodhihirisha Imani na kuficha ukafiri- kuwa wao watakuwa na adhabu yenye kuumiza.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net