An-Nisaa 4:137
النساءإِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ثُمَّ كَفَرُوا۟ ثُمَّ ءَامَنُوا۟ ثُمَّ كَفَرُوا۟ ثُمَّ ٱزْدَادُوا۟ كُفْرًا لَّمْ يَكُنِ ٱللَّهُ لِيَغْفِرَ لَهُمْ وَلَا لِيَهْدِيَهُمْ سَبِيلًۢا
Hakika, wale walioamini, kisha wakakufuru, kisha wakaamini, kisha wakazidi ukafiri, Mwenyezi Mungu hakuwa wa kuwafutia dhambi wala wa kuwaongoa njia.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika walio amini, kisha wakakufuru, kisha wakaamini, kisha wakazidi ukafiri, Mwenyezi Mungu hakuwa wa kuwaghufiria wala wa kuwaongoa njia. [137]
[137] Hakika Imani ni kuit'ii Haki kusio kuwa na ukomo, na kunako endelea daima. Basi wanao taradadi wakababaika si Waumini. Hao ambao wanaamini, kisha wakakufuru, kisha wakaamini, kisha wakakufuru, na kwa hivyo wakazidi ukafiri wao - Mwenyezi Mungu hatakuwa wa kuwaghufiria watu hao hivyo vitendo vyao viovu, wala hatawaongoa kwenye Haki. Kwani kusamehe kwa Mwenyezi Mungu kunahitajia toba, na kujing'oa na shari, na uwongofu wake ni kwa wale wanao ielekea Haki na wanaitaka.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika wale walioingia kwenye Imani, kisha wakarudi kwenye ukafiri, kisha wakarejea kwenye Imani, kisha wakarudi tena kwenye ukafiri, kisha wakazama na kuendelea kwenye ukafiri, Allah Mtukufu Hatakuwa ni Mwenye kuwasamehe wala kuwaonesha njia ya uongofu ambayo kwayo wataokoka na mwisho mbaya.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net