An-Nisaa 4:136
النساءيَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ ءَامِنُوا۟ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ وَٱلْكِتَـٰبِ ٱلَّذِى نَزَّلَ عَلَىٰ رَسُولِهِۦ وَٱلْكِتَـٰبِ ٱلَّذِىٓ أَنزَلَ مِن قَبْلُ ۚ وَمَن يَكْفُرْ بِٱللَّهِ وَمَلَـٰٓئِكَتِهِۦ وَكُتُبِهِۦ وَرُسُلِهِۦ وَٱلْيَوْمِ ٱلْـَٔاخِرِ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَـٰلًۢا بَعِيدًا
Enyi mlioamini! Muaminini Mwenyezi Mungu, na Mtume wake, na Kitabu alichokiteremsha juu ya Mtume wake, na Kitabu alichokiteremsha kabla yake. Na anayemkufuru Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake, na Mitume wake, na Siku ya Akhera, basi hakika amekwishapotea kupotea kwa mbali.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Enyi mlio amini! Muaminini Mwenyezi Mungu, na Mtume wake, na Kitabu alicho kiteremsha juu ya Mtume wake, na Kitabu alicho kiteremsha kabla yake. Na anaye mkataa Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake, na Mitume wake, na Siku ya Akhera, basi huyo amekwisha potelea mbali. [136]
[136] Kwa hakika Ujumbe wa mbinguni ni mmoja, kwa kuwa yule Mwenye kutuma ni Mmoja, naye ni Mwenyezi Mungu. Basi enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu na mumsafie niya. Na msadikini Mtume wake Muhammad, na msadiki yaliyo kuja katika Kitabu chake alicho mteremshia, na mtende yaliyo amrishwa humo. Na sadikini Vitabu vilivyo teremshwa kabla yake kama alivyo teremsha Mwenyezi Mungu bila ya mageuzo wala kusahau. Aminini yote hayo. Kwani mwenye kumkanusha Mwenyezi Mungu, Muumba wa viumbe vyote, na Malaika, na Mwenye kuyajua yaliyo fichikana, na Vitabu vya Mwenyezi Mungu na Mitume wake, na akaikanusha Siku ya Mwisho, basi huyo ameipotea Njia Iliyo Nyooka, na ametokomea mbali katika njia ya upotovu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Enyi mliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkafuata sheria Zake kivitendo, endeleeni kwenye msimamo mlionao wa kumuamini Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Imani thabiti, kumuamini Mtume Wake Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, na kuwatii wao wawili, kuiamini Qur’ani Aliyoiteremsha kwake na kuviamini vitabu vyote Alivyoviteremsha Allah Mtukufu kwa Mitume. Na mwenye kumkanusha Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Malaika Wake waliotukuzwa, vitabu Vyake Alivyoviteremsha ili kuwaongoza viumbe Wake, Mitume Wake Aliowachagua kufikisha ujumbe Wake na Siku ya Mwisho ambayo watu katika siku hiyo watafufuka baada ya kufa ili waorodheshwe na wahesabiwe, atakuwa ametoka kwenye Dini na atakuwa yuko mbali sana na njia ya haki.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net