Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 135

An-Nisaa 4:135

النساء

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ كُونُوا۟ قَوَّٰمِينَ بِٱلْقِسْطِ شُهَدَآءَ لِلَّهِ وَلَوْ عَلَىٰٓ أَنفُسِكُمْ أَوِ ٱلْوَٰلِدَيْنِ وَٱلْأَقْرَبِينَ ۚ إِن يَكُنْ غَنِيًّا أَوْ فَقِيرًا فَٱللَّهُ أَوْلَىٰ بِهِمَا ۖ فَلَا تَتَّبِعُوا۟ ٱلْهَوَىٰٓ أَن تَعْدِلُوا۟ ۚ وَإِن تَلْوُۥٓا۟ أَوْ تُعْرِضُوا۟ فَإِنَّ ٱللَّهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا

Maana

Enyi mlioamini! Kuweni wenye kusimama imara katika kufanya uadilifu, wenye kushuhudia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, hata kama ni juu ya nafsi zenu, au wazazi wawili na jamaa zenu. Akiwa tajiri au fukara, Mwenyezi Mungu ndiye anayewastahiki zaidi. Basi msifuate matamanio, mkaacha kufanya uadilifu. Na mkiupotoa au mkaupa mgongo, basi Mwenyezi Mungu anajua vyema mnayoyatenda.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi mlio amini! Kuweni wenye kusimamisha uadilifu, mtowao ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, ijapo kuwa ni juu ya nafsi zenu, au wazazi wawili na jamaa zenu. Akiwa tajiri au masikini Mwenyezi Mungu anawastahikia zaidi. Basi msifuate matamanio, mkaacha kufanya uadilifu. Na mkiupotoa au mkajitenga nao basi Mwenyezi Mungu anajua vyema mnayo yatenda. [135]

[135] Uadilifu ndio nidhamu ya maumbile. Na hiyo ndiyo sharia ambayo haiwezi kuwapo ndani yake maoni ya kukhitalifiana. Basi enyi mlio mt'ii Mwenyezi Mungu wa Haki, na wito wa Mitume wake, kuweni macho nafsi zenu katika kuut'ii uadilifu, na kuweni macho kwa ajili ya watu. Mfanyieni insafu aliye dhulumiwa, na msimame imara, si kwa ajili ya kumpendelea tajiri, au kumwonea huruma masikini. Kwani Mwenyezi Mungu aliye waumba matajiri na masikini anastahiki zaidi kuangalia hali ya tajiri au fakiri. Matamanio ndiyo yanayo mpelekea mtu kumili nafsi yake, basi msiyafuate matamanio mkaacha uadilifu. Na mkikengeuka mkaacha uadilifu, au mkapuuza kusimamisha uadilifu, basi mjue Mwenyezi Mungu anayajua myatendayo, tena anayajua kwa ujuzi wa ndani. Naye atakulipeni kwa mujibu wa a'mali yenu; ikiwa njema mtalipwa wema, ikiwa ovu mtalipwa shari.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi mliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkafuata sheria Zake kivitendo, kuweni ni wasimamizi wa uadilifu, wenye kutekeleza ushahidi kwa ajili ya Allah Mtukufu, hata kama ni kinyume na maslahi ya nafsi zenu au baba zenu au mama zenu au jamaa zenu, na vyovyote atakavyokuwa yule mwenye kutolewa ushahidi awe ni tajiri au masikini, kwani Allah Mtukufu ni bora kwa wao wawili kuliko nyinyi, na ni Mjuzi zaidi wa mambo ambayo yana maslahi kwao. matamanio na mapendeleo yasiwapelekee nyinyi kuacha uadilifu. Na mkiupotoa ushahidi, kwa ndimi zenu, mkautoa kwa namna isiyokuwa ya kweli, au mkaupuuza kwa kuacha kuutekeleza au kwa kuuficha. Hakika Allah Mtukufu ni Mjuzi wa matendo yenu ya ndani na Atawalipa kwayo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net