An-Nisaa 4:134
النساءمَّن كَانَ يُرِيدُ ثَوَابَ ٱلدُّنْيَا فَعِندَ ٱللَّهِ ثَوَابُ ٱلدُّنْيَا وَٱلْـَٔاخِرَةِ ۚ وَكَانَ ٱللَّهُ سَمِيعًۢا بَصِيرًا
Mwenye kutaka malipo ya dunia, basi kwa Mwenyezi Mungu yapo malipo ya dunia na Akhera. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia vyema, Mwenye kuona yote.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Anaye taka malipo ya dunia, basi kwa Mwenyezi Mungu yapo malipo ya dunia na Akhera. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia na Mwenye kuona. [134]
[134] Na watu, pindi wakitafuta neema za dunia zilizo halali kwa njia ya haki iliyo nyooka sawa, basi hakika Mwenyezi Mungu atawapa neema za duniani na Akhera; kwani Yeye ndiye aliye miliki neema zote mbili.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Mwenye kuwa na hamu miongoni mwenu, enyi watu, ya kupata malipo ya duniani na akaipa mgongo Akhera, basi mbele ya Allah Mtukufu kuna malipo ya dunia na Akhera. Basi na atake kutoka kwa Allah Mtukufu, Peke Yake, wema wa dunia na Akhera, kwani Yeye Ndiye Anayevimiliki hivyo viwili. Na Allah Mtukufu ni Mwenye kuyasikia maneno ya waja Wake, ni Mwenye kuziona nia zao na vitendo vyao, na Atawalipa kwa hayo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net