An-Nisaa 4:133
النساءإِن يَشَأْ يُذْهِبْكُمْ أَيُّهَا ٱلنَّاسُ وَيَأْتِ بِـَٔاخَرِينَ ۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلَىٰ ذَٰلِكَ قَدِيرًا
Akitaka, atawaondoa, enyi watu! Na awalete wengineo. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza mno wa hayo.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Akitaka atakuondoeni, enyi watu! Na awalete wengineo. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa hayo. [133]
[133] Hakika nyinyi enyi waja wa Mwenyezi Mungu! Mko chini ya ufalme wa Mwenyezi Mungu Mwenye uweza na Mwenye nguvu. Akipenda atakufisheni na alete wengine kabisa. Na Yeye Mwingi wa Utukufu ni Muweza wa hayo, na Muweza wa kila kitu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Akitaka Allah Mtukufu Atawaangamiza, enyi watu, na awalete watu wengine wasiokuwa nyinyi. Na Allah Mtukufu kwa hili ni Muweza.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net