An-Nisaa 4:132
النساءوَلِلَّهِ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَمَا فِى ٱلْأَرْضِ ۚ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ وَكِيلًا
Na ni vya Mwenyezi Mungu vilivyo katika mbingu na vilivyo katika ardhi. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Mtegemewa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na ni vya Mwenyezi Mungu viliomo katika mbingu na viliomo katika ardhi. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Mlinzi. [132]
[132] Kupanga kila kitu cha mbinguni na duniani ni kazi ya Mwenyezi Mungu Aliye takasika na Aliye tukuka. Yeye ndiye Mwenye madaraka, Mwenye kuendesha, Mwenye kupanga. Yatosha kuwa Yeye ndiye Mtawala aliye amrisha ulimwengu ukajipanga ulivyo jipanga, na akawaamrisha watu wamuabudu, na wamtegemezee Yeye mambo yao, na wamche Yeye.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ni milki ya Allah Mtukufu viumbe vilivyoko mbinguni na arohini. Na inatosha kuwa Yeye, Aliyetakasika na kila sifa pungufu, ni Msimamizi na Mtunzi wa mambo ya viumbe Vyake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net