Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 131

An-Nisaa 4:131

النساء

وَلِلَّهِ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَمَا فِى ٱلْأَرْضِ ۗ وَلَقَدْ وَصَّيْنَا ٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ ٱلْكِتَـٰبَ مِن قَبْلِكُمْ وَإِيَّاكُمْ أَنِ ٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ ۚ وَإِن تَكْفُرُوا۟ فَإِنَّ لِلَّهِ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَمَا فِى ٱلْأَرْضِ ۚ وَكَانَ ٱللَّهُ غَنِيًّا حَمِيدًا

Maana

Na ni vya Mwenyezi Mungu tu vyote vilivyo katika mbingu na vilivyo katika ardhi. Na kwa hakika tuliwausia wale waliopewa Kitabu kabla yenu, na nyinyi pia, kwamba mumche Mwenyezi Mungu. Na mkikufuru, basi ni vya Mwenyezi Mungu vilivyo katika mbingu na vilivyo katika ardhi. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosheleza, Msifiwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na ni vya Mwenyezi Mungu tu vyote viliomo katik mbingu na viliomo katika dunia. Na kwa hakika tuliwausia walio pewa Kitabu kabla yenu, na nyinyi pia, kwamba mumche Mwenyezi Mungu. Na mkikataa, basi ni vya Mwenyezi Mungu viliomo mbinguni na viliomo duniani. Na Mwenyezi Mungu ni Mkwasi, anajitosha, na Msifiwa. [131]

[131] Kiini cha Dini ni kumnyenyekea Mwenye kuumba ulimwengu, Mwenye utukufu na ukarimu, na kuukubali ufalme wake usio na ukomo. Kwani ni vya Mwenyezi Mungu vyote viliomo mbinguni na katika ardhi. Na kwa huu Ufalme usio na ukomo amesema: Tumewausia watu wa dini zilizo toka mbinguni, katika Watu wa Kitabu na nyinyi Waislamu, mumkhofu Mwenyezi Mungu, na mumuabudu Yeye, na msiwe mnakufuru katika ibada yake, maana Yeye ndiye Mwenye utawala mkubwa kushinda wote. Hapana kitu kilicho toka nje ya utawala wake. Yeye ni Mkwasi, yaani mwenye kujitosha wala hakuhitajiini nyinyi. Juu ya hivyo Yeye anakuhimidini kwa imani yenu, kwani kwa kuwa Yeye ni Mwenye kujitosheleza mwenyewe, juu ya hivyo anasifu na kushukuru vitendo vyema vya waja wake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ni milki ya Allah Mtukufu vilivyoko kwenye mbingu na vilivyoko kwenye ardhi na vilivyoko baina ya hivyo viwili. Na tuliwausia wale waliopewa Vitabu kabla yenu, miongoni mwa Mayahudi na Wanaswara, na tukawausia nyinyi pia, enyi ummah wa Muhammad, mumche Allah Mtukufu, Aliyetukuka, na msimame katika kutekeleza amri Zake na kuepuka makatazo Yake, na tukawaelezea kwamba nyinyi mkiukanusha upweke wa Allah Mtukufu, Aliyetukuka, na sheria Zake, basi Allah Mtukufu Hawahitajii nyinyi, kwa kuwa vyote vilivyoko kwenye mbingu na vilivyoko kwenye ardhi ni Vyake. Na Allah Mtukufu ni Mwenye kujitosha kutowahitjia viumbe Wake, ni Mwingi wa kuhimidiwa katika sifa Zake na vitendo Vyake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net